Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari?
Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari?
Hapana kiwango maalum cha mahari kilichowekwa na Sheria ya Kiislamu. Mahari ni haki ya mwanamke mwenye kuolewa na ndiye pekee mwenye uhuru kamili wa kutaja kiasi cha mahari anachokitaka. Akipenda anaweza kudai mrundi wa dhahabu na fedha (Qur-an: 4:20), au akitaka anaweza kupokea kiasi kidogo sana cha mali kama vile shilingi 1/- au chini zaidi kuliko hivyo au akitaka anaweza akasamehe asitake kitu chochote ila kauli nzuri tu.
Lakini tunashauriwa katika Qur-an kuwa mtoaji mahari na mpokeaji mahari waangaliane hali. Kama hali ya mtoaji ni nzuri, ni vyema azidishe mahari kuliko kile kiasi kilichotajwa iwapo ana uwezo huo. Na mpokeaji wa mahari, endapo ataona hali ya mtoaji si nzuri kiuchumi, basi ampunguzie mahari na apokee kiasi kidogo zaidi ya kile alichokitaja mwanzoni. Huku kuangaliana hali kunazidisha mapenzi na huruma baina ya mume na mke.
Pamoja na kuwa mahari hayana kiwango maalum kilichowekwa, inashauriwa yasiwe ya juu sana kiasi cha kuifanya ndoa kuwa jambo gumu na kurahisisha uzinifu katika jamii. Hebu tuusikilize ushauri wa Umar bin Khattab (r.a) (Khalifa wa Pili wa Mtume (s.a.w) ambaye amesema:
"Kuweni waangalfu msfanye mahari ghali. Ingelikuwa kufanya hivyo ni jambo zuri la kumpelekea mtu kwenye ucha-Mungu, Mtume (s.a.w) angelikuwa wa kwanza katikajambo hilo. Sikumbuki kumuona Mtume (s.a.w) katika lwmuoa yeyote katika wake zake au katika lwwaoza yeyote katika binti zake kwa zaidi ya Wakia 12.5 (lwmi na mbili na nusu) ambazo ni sawa na Dirham 500".
Pia katika hadithi iliyosimuliwa na Jabir (r.a) Mtume (s.a.w) amesema: Atakayetoa viganja viwili vya tende au shairi kama mahari ya mkewe (naye akaridhia) atakuwa ameufanya uchi wa mkewe uwe halali kwake. (Abu Daud).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 312
Sponsored links
π1 kitabu cha Simulizi
π2 Simulizi za Hadithi Audio
π3 Kitabu cha Afya
π4 Madrasa kiganjani
π5 Kitau cha Fiqh
π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
quran na sayansi
Soma Zaidi...
HADITHI 40 ZA IMAMU NAWAWI: haithi za Mtume (s.a.w) 40 zilizoandikwa na Imam Nawaw)
Soma Zaidi...
Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa
Soma Zaidi...
Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii
1. Soma Zaidi...
Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...
Madai ya Makafiri Dhidi ya Qurβan na Udhaifu Wake
i. Soma Zaidi...
ushahidi juu ya Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W)
Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S. Soma Zaidi...
nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...
Mafunzo ya Sura Zilizochaguliwa
Soma Zaidi...
MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...