7.
7. Kulala Muzdalifa
Muzdalifa ni kitongoji kilichoko kati ya Arafa na Mina. Baada ya jua kuchwa Mtume (s.a.w) na Waislamu waliongozana nao katika Hija ya kuaga, waliondoka Arafa na kuelekea Muzdalifa kwa kufuata njia tofauti na ile waliyoijia kutoka Mina.
Wakati wa kwenda Muzdalifa, Mtume (s.a.w) amewaamrisha Waislamu waende kimya kimya katika mwendo wa utulivu bila ya makelele na vishindo.Mtume (s.a.w) na Waislamu alioongozana nao waliswali al-Magharibi pamoja na al-Ishai kwa Qasr walipofika Muzdalifa. Mtume (s.a.w) na Waislamu walilala Muzdalifa mpaka Alfajir, bali Mtume (s.a.w) aliwaruhusu watu dhaifu pamoja na wanawake na watoto waondoke kwenda Mina usiku wa manane baada ya mwezi kutua ili waende pole pole na kuepukana na msongamano wa watu wakati wa kutupa mawe. Lakini aliwaamuru wasianze kutupa mawe mpaka jua lichomoze. Baada ya swala ya Al-fajir, Mtume (s.a.w) alipanda ngamia na kuelekea sehemu takatifu iitwayo “Mash-arul-Haram”. Ilivyo ni kwamba bonde lote la Muzdalifa linaitwa kwa jina hili lakini sehemu hasa ambayo Mtume (s.a.w) alisimama katika hija ya Kuaga ni pale ulipo Msikiti wa Muzdalifa hivi sasa. Mtume (s.a.w) alipofika hapa “Mash-arul Haram” alielekea Qibla, akatoa Takbira na kumuomba Allah (s.w).Haya ndio maagizo ya Allah (s.w) kama tunavyosoma:
“.Na mtakaporudi kutoka Arafaat m tajeni Mw enyezi Mungu kw enye Mash-arul Haram. Namkumbukeni kama alivyokuongozeni. Na hakika zamani mlikuw a miongoni mwa waliopotea ” (2:198).
Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba si lazima kila Haji asimame sehemu ya Msikiti, bali sehemu yoyote atakayosimama wakati huu wa kumtukuza Allah (s.w) kwa Takbira na kuomba dua, itafaa ili mradi tu aelekee Qibla. Kwani kama tulivyoona katika hadith, Mtume (s.a.w) amesema:
“Ninasimama hapa lakini bonde lote la Muz-dalifa ni mahali pakukaa na kusimama ” (Muslim).
Baada ya jua kuchomoza, Mtume (s.a.w) na mahujaji wengine walianza safari ya kuelelekea Mina. Walipofika kwenye bonde la Muhassir (mahali walipouawa watu wenye jeshi la tembo), Mtume (s.a.w) aliwaamuru watu wapite haraka haraka. Wakati wakielekea Mina Mtume (s.a.w) alimtuma Fadhl bin Abbas (r.a) amuokotee vijiwe saba na akawaamuru watu wengine waokote vijiwe saba. Mahali popote pale njiani kuelekea Mina isipokuwa kwenye bonde la Muhassir mtu anaweza kuokota vijiwe saba kwa ajili ya ibada ya kutupa mawe kwenye mnara mkubwa (Jamaratul Aqaba). Mtume (s.a.w) alikuwa akiitikia Labbayka (Talbiya) kuanzia Muzdalifa mpaka alipofika Mina na kuanza kutupa jiwe la kwanza kwenye mnara mkubwa kama tunavyojifunza katika hadith ifu atayo:
Ames imulia Ibn Abbas (r.a): Mtume (s.a.w) alimpandisha Al-Fadhl katika kipando chake na akaw a nyuma yake, na Fadhl ameeleza kuw a Mtume (s.a.w) aliendelea mfululizo kuleta Talbiya mpaka alipofanya Ramy katika Jamrat (Jamratul Aqaba). (Bukhari).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 331
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Madrasa kiganjani
Taratibu za kumuona mchumba
Soma Zaidi...
Makundi ya dini zilizotajwa kwenye quran na athari zake katika jamii
2. Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...
Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...
Namna ya kuswali swala ya kuombea haja
9. Soma Zaidi...
NASAHA ZANGU NNE KWAKO KUHUSU QURAN, MAUTI, DUA NA MENGINE
Soma Zaidi...
Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...
Taratibu za kufunga ndoa na kumuinglia mke
Soma Zaidi...
namna ya kuswali swala ya dhuha
7. Soma Zaidi...
DARSA ZA QURAN
DARSA ZA QURAN 1. Soma Zaidi...
Lengo la swala
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Soma Zaidi...