Zoezi

Zoezi

Maswali mbalimbali yanayohusu elimu ya dini ya kiislamu na mwongozo wa elimu na elimu mazingira.

Zoezi la 1.

1.(a)  Elimu ni nini?

(b)  Mtu aliyeelimika ni mtu wa aina gani?

(c)  Unatoa maoni gani iwapo wanaojua watakuwa sawa na wasiojua kiutendaji?

 

2.(a)  “….Sema, Je! Wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?.....(39:9).   Kwa nini wanaojua hawawi sawa na wasiojua?

(b) Kwa kutumia ushahidi wa aya, onesha kuwa elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

 

3.Kwa ushahidi wa aya za Qur’an, eleza kwa nini Uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza kabla ya jambo lolote?

 

4.(a)  Nini chanzo cha elimu na fani zote?

(b)  “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba…….” (96:1).

      (i)  Kutokana na aya hii, fafanua nini maana ya kusoma ‘kwa jina la Allah’

      (ii) Orodhesha njia tano anazotumia Allah (s.w) katika kuwaelimisha wanaadamu.

 

5 (a)  Bainisha ni upi mgawanyo sahihi na usio sahihi juu ya elimu katika Uislamu.

(b) Tofautisha kati ya elimu ya mwongozo(faradh ‘Ain) na elimu ya mazingira (faradh kifaya).

 

6.‘Mgawanyo wa Elimu Dunia na Akhera (dini) haukubaliki (haupo) katika Uislamu’. Eleza ni kwa nini kwa kutoa sababu zisizopungua tano.

 

7.(a)   Ni ipi elimu yenye manufaa?

(b)  Eleza kwa ufupi, kwa nini ili Uislamu usimame katika jamii, hatuna budi kutotenganisha ‘Elimu ya Mwongozo na Elimu ya Mazingira’?

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views: 3246

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 web hosting     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

(xiii)Huwa muaminifu

Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana.

Soma Zaidi...
Neno la awali

Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.

Soma Zaidi...
KULA HALALI NA ZILICHO KIZURI NI AMRI KATIKA UISLAMU

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَي...

Soma Zaidi...