23.
23. Kuwa mwenye Huruma
Muumini hana budi kujipamba na tabia ya kuwahurumia viumbe wenzake. Amuoonee huruma kila mwenye shida na ajitahidi kumsaidia iwezekanavyo. Katika kuonesha umuhimu wa kipengele hiki cha tabia njema Mtume (s.a.w) amesema:
โAmbaye hahurumii watu, pia Allah (s.w) hatamuhurumia โ. (Bukhari).
Huruma hudhihiri katika kuwasaidia wenye shida na matatizo kwa mali na kauli njema kama tunavyojifunza katika Qur-an:
โHamtaweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vitu mnavyovipenda, na chochote mnachokitoa, basi hakika Allah anakijua โ. (3:92).
โSio wema (tu) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi. Bali wema (hasa) ni (wale) wanaomwamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, w anawapa mali, juu ya kuwa wanayapenda, jamaa na mayatima na maskini na wasafiri (w alioharibikiwa) na waombao na katika kuwakomboa watumwa...โ (2:177
โโฆ Na wafanyie wema wazazi na jamaa na yatima na maskini na semeni na watu kwa wemaโฆโ (2:83).
Pamoja na kuonyesha huruma kwa wanaadam wenzetu, Uislamu pia umetutaka tuwe na huruma kwa wanyama. Tunafahishwa katika hadith kuwa mtu mmoja alimuambia Mtume:
Ee Mtume w a Allah! Ninapochinja mbuzi ninajaribu kumuonea huruma. Mtume (saw) akasema: โKama utamuonea huruma , Huruma ya Allah itakuwa juu yakoโ. (Hakim)
Pia katika hadith nyingine Mtume (saw) amesema:
โMwanamke mkosefu alimuona mbwa akiwa anachungulia kisima, siku ya joto kali na ulimi wake ukiwa umeningโinia kuonyesha kiu kali aliyokuwa nayo. Alimuonea huruma na akamtekea maji na chombo chake. Kutokana na kitendo chake hiki (cha kumuhurumia mbwa), alipata uokovuโ. (Muslim)
Pia Hadith ifuatayo inatuonyesha kuwa waislam wanatakiwa
wanyooshe mkono wa huruma kwa viumbe vyote vilivyo hai. Mtume (saw) amesema:
โWahurumie waliomo ardhini, na yule aliyopo mbinguni atawamiminia huruma yakeโ
Kinyume chake kuwa katili kwa wanyama ni kitendo cha dhambi kinachoweza kumuingiza mtu motoni. Mtume (saw) amesema:
Mwanamke alitiwa motoni kwa sababu alimfunga paka bila ya kumlisha au kumwachia huru, ambapo angaliweza kwenda huku na huku na kujilisha kutokana na wadudu , n.k. (Bukhari)
Kutokana na Hadith hizi tujue kuwa Allah (sw) hata turehemu iwapo tutakuwa wakatili kwa wanaadamu wenzetu na viumbe wengine.
Umeionaje Makala hii.. ?
ุนููู ุฃูุจูู ุญูู ูุฒูุฉู ุฃูููุณู ุจููู ู ูุงูููู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฎูุงุฏูู ู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ุนููู ุงููููุจูููู ุตูู ุงููู ุนููู ?...
Soma Zaidi...Kipengele hichi kina maswali mbalimbali kuhusiana na dini na mitazamo mbalimbali.
Soma Zaidi...2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA
Soma Zaidi...