33. Kuepuka Tamaa na KuombaombaKinyume cha kutosheka ni kuwa na tamaa au kutotosheka. Kutotosheka ni ufakiri wa moyo. Moyo wa kutotosheka huzaa tabia nyingi mbaya ikiwa ni pamoja na upupiaji mali, husuda, uchoyo, na kuomba omba. Muislamu anatakiwa ajitahidi kutosheka na alichonacho na hata kama anahisi yuko katika dhiki ajitahidi kujizuilia kunyoosha mkono wa kuomba chochote kwa yeyote kwa kadiri iwezekanavyo.
Tumekatazwa katika Qur-an kutamani vitu vya watu:


“Wala msitam ani vile am bavyo Mw enyezi Mungu am ew afadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma; na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile


w alivyovichuma;. Na mw ombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (4:32).
Kuhusu suala la omba omba Mtume (s.a.w) ametuusia katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule aombaye ili aongezee mali yake, haombi lingine ila moto wa maisha. (Muslim).
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Kama mmoja wenu ataomba bila ya sababu ya msingi atakutana na Allah na uso usiokuwa na nyama ”. (Bukhari na Muslim)Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alipokuwa Mimbarini akitoa khutba juu ya kutoa sadaqa na kujizuia na kuomba omba alisema: “Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Mkono wa juu ni ule unaotoa na wa chini ni ule unaoomba”. (Bukhari na Muslim).
Kuomba kunaruhusiwa kwa dharura zifuatazo:(i)Mtu aliyesimama kumdhamini mtu mwingine ili kuleta suluhu kati ya wagomvi wawili huyu anaruhusiwa kuomba hata akiwa tajiri. Kwa mnasaba huu, wadhamini wa Misikiti, madrasa, na shughuli mbali mbali za Kiislamu wanaruhusiwa kuomba michango ya Waislamu ili kufanikisha shughuli hizo.
(ii)Mtu aliyepata ajali na kuharibikiwa kabisa vitu vyote kama vile ajali ya moto, mafuriko, n.k.(iii)Mtu ambaye amepigwa na ufukara na amekosa kabisa mahitaji muhimu ya maisha kama chakula, malazi na makazi. Lakini mtu akiwa kama na angalau chakula cha siku moja na malazi na akawa na dirham 50 mkononi mwake haruhusiwi kuomba kama tunavyofahamishwa katika Hadithi zifuatazo:Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Anayeomba omba watu na ilhali ana mahitaji muhimu ya maisha atakuja siku ya Kiyama na kuomba omba kwake kama mikwaruzo, vidonda au majeraha usoni mwake. Iliulizwa: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni kiasi gani kinachomtosha mtu? Akajibu: Dirham 50 au thamani yake ya dhahabu (Abu Daud, Tirmidh, Nasai na Ibn Majah)Sahl (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule anayeomba na ilihali anajitosheleza kw a mahitaji muhimu, anaomba


moto (Jahannam). Nufali (r.a) ambaye ni miongoni mwa wasimulizi wa hadithi hii katika sehemu nyingine aliuliza: Ni yupi mwenye uwezo ambaye kuomba ni haram? Akajibu Mtume (s.a.w): Yule mwenye uwezo wa kupata chakula cha asubuhi na usiku. Mahali pengine amesema: Yule mwenye chakula cha siku moja (Usiku na mchana). (Abu Daud).