BAADA YA KUZIKA NINI KIFANYIKE


Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo. Baada ya kumzika maiti sasa kuna utaratibu utafanyika. Watu ambao wamebaki duniani bado wana nafasi ya kumsaidi maiti akiwa kaburini, kumsadia kwa heri ama kwa shari. Makala hii inakwenda kukuorodheshea mambo kadhaa ambayo ni muhimu kwa waliohai kuyafanya baada ya kumzika ndugu yao:

Nini tufanye baada ya kuzika:
1.Kumuombea dua marehemu, dua hii anaweza kuombewa na watoto wake, ndugu zake, wake zake ama yoyote anaye mfahamu
2.Kuzungumza mema ya marehemu na kuwacha kuzungumza maovu yake.
3.Kumlipia madeni yake
4.Kuwafariji ndugu na familia ya marehemu
5.Kuwapikia chakula wafiwa
6.Kutekeleza usia wake baada ya kulipa madeni
7.Kurithisha mali yake baada ya kulipa madeni na kutekeleza usia
8.Kumtolea sadaka
9.Kum;ipia baaadhi ya ibada zake kama hija na swaumu
10.Kumhijia
11.Kuzuru kaburi lake
12.Kumuombea dua pindi unapomkumbuka
13.Kufanya wma katika mali zake