picha

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)

Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema.

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)

MAANDALIZI BINAFSI KABLA YA KUFA



Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema. Maandalizi haya yanaweza kuwa kabla ya kuumwa ama wakati wa kuumwa. Pia maandalizi haya yanaweza kuwa ni ya muda mrefu kabla ya kufa ama sekunde chache kabla ya kuumwa. Kwa ufupi makala hii itakueleza maandalizi haya kwa kuyaorodhesha tu.


Maandalizi binafsi kabla ya kufa:
1.Kufanya mambo mema na kwacha mambo maovu.
2.Kutoa usia katika mali zako, na utaratibu wa usi ni kuwa hutahusia katika mali yako kiasi kitakachoziki theluthi, pia hutamuhusia katika mali yako mtu anayekurithi. Pia hakikisha kuwa unafanya uadilifu katika kuhusia. Na katu usihusie mambo maovu.
3.Kulipa madeni inapowezekana.
4.Kutubua madhambi, toba itakubalika muda wowote kabla ya kutoka kwa roho. Inakupasa kuzijuwa sharti za toba na namna ya kutubia. Toba inakubaliwa kwa madhambi yote uliyoyafanya kwa siri ama kwa dhahiri, makubwa na madogo.
5.Kuleta adhkari muda mwingi na kumkumbuka Allah. Kufanya istighfas wakati mwingi. Hii itakukurubisha kwa Allah zaii na kufanya matendo yako mema yakubaliwe.
6.Kuwa na subira, kuridhika na kumdhania mema Allah.
7.Katu usitamani kufa, kutamani kufa kumekatazwa katika uislamu.
8.Tembelea wagonjwa ukiweza, na tumia muda kuyafikiria mauti.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 2365

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 ai web app    

Post zinazofanana:

fadhila za kusoma quran

Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1.

Soma Zaidi...
NGUZO ZA IMAN

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...