ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

Ihram



Mwenye kunuia Hija au 'Umra katika Miiqaat anakuwa katika hali ya kuchunga masharti kadhaa mpaka akamilishe matendo kadhaa ya Hija au 'Umra. Hali hii ya kuchunga masharti hujulikana kwa jina la 'Ihram '.



Wanaume wanapokuwa katika Ihram hulazimika kuvaa vazi rasmi la Ihram.Vazi la Ihram kwa wanaume ni kuvaa shuka mbili nyeupe zisizo shonwa.Shuka moja hufungwa kiunoni na mkanda huweza kutumika ili kuhakikisha isivuke. Shuka la pili huvaliwa lubega kwa kufunika bega la kulia na kuacha wazi bega la kushoto. Katika hali ya Ihram, ni haram kwa mwanamume kuvaa nguo nyingine yoyote, ni haramu kufunika kichwa, ni haram kuvaa soksi au kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Wanawake hawana vazi rasmi la Ihram. Akiwa katika Ihram Hajat analazimika kama kawaida kujifunika mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono na atavalia ushungi. Hijab yaweza kuwa ya rangi yoyote isiyovutia kama kawaida ya vazi la mwanamke wa Kiislamu lakini vazi jeupe ni bora. Mwanamke akiwa katika Ihram ni haramu kufunika uso au kuvaa soksi za mikononi(gloves). Pia wanawake katika Ihram hawaruhusiwi kuvaa soksi wala kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Yaliyoharamishwa kwa Mwenye kuwa katika Ihram
(i)Kujimai (kufanya tendo la ndoa) au kubusu au kukumbatiana au kufanya vitendo vingine vya kimapenzi kati ya mume na mke ambavyo vitawaletea fikra za kufanya ten do la ndoa.
(ii)Kusema maneno maovu na machafu kama vile kusengenya,kugombana, kugombanisha, kusema uwongo, kubishana, n.k. Na anayekusudia kufanya Hija katika (miezi) hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija ... (2:197).
(iv) Kunyoa au kung'oa nywele, kukata kucha au kukata au kupunguza sehemu yoyote ya mwili ila kwa matibabu kama vile kuumika, kutolewa damu kwa ajili ya matibabu na mengineyo.
(vi)Kuoa au kufanya mipango ya ndoa au hata kupeleka posa.
(vii)Kujipaka manukato
(viii)Kuvaa nguo ya rangi yenye kuvutia
(ix)Kwa wanaume kuvaa nguo iliyoshonwa, na kufunika kichwa.
(x)Kwa wanawake kufunika uso na kufunika viganja vya mikono kwa kuvaa glovu (gloves).
(xi)Kuvaa viatu vinavyofunika miguu na kuvaa soksi.
(xii)Kuwinda au kusaidia kuwinda angalau kwa kuonyesha mnyama anayewindwa.
(xiii)Kula nyama iliyowindwa au iliyopatikana kwa msaada wa mtu aliyekuwa katika Ihram.
(xiv)Kula mayai ya ndege waliopatikana kwa kuwindwa.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 236


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-