Kafara kwa mwenye kuvunja masharti ya IhramAllah (s.w) kwa Urehemevu wake, ametoa nafuu kwa wale watakaovunja masharti ya Ihram kwa kutoa fidia isipokuwa kwa kosa la jimai.Tunafahamishwa katika Qur-an:


“... Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana vya kumuudhi kichw ani mw ake (akafanya yaliyokatazw a, kama vile kunyoa), basi atoe fidia kwa kufunga au (kwa kutoa) sadaqat au kuchinja mnyama ...” (2:196)


Katika Hadith tunafahamishwa:
Ka’ab bin Ajra (r.a) ameeleza: “Nilipokuwa katika (hali ya) Ihram kwa ajili ya ‘Umra nilisumbuliwa sana na chawa kichwani mwangu. Mtume wa Allah (s.a.w) akaniambia ninyoe kisha nifunge siku tatu au nichinje mbuzi wa sadaqat au niwalishe maskini sita. (Bukhari, Muslim, Abu Da ud).
Kwa hiyo kwa Muharim atakayevunja sharti lolote la Ihram atalazimika kutoa kafara kwa ama


(i) kufunga siku 3 au


(ii) kumchinja mbuzi na kuitoa nyama yake sadaqat au


(iii) kulisha maskini sita.Kumwingilia mke ni kosa lisilosameheka kwa kutoa kafara bali hubatilisha Hija au ‘Umra moja kwa moja. Ama kwa mume aliyefanya mapenzi na mkewe kwa kubusiana na kumkumbatia bila ya kufanya kitendo cha ndoa, atatoa kafara ya ngamia (au thamani yake) kama atatokwa na manii na kama hatatokwa na manii, atatoa kafara ya mbuzi.
Kafara kwa mwenye kuwinda au kuonyesha windo akiwa katika Ihram ni mbuzi iwapo mnyama huyo ana ukubwa wa mbuzi, au mdogo zaidi kuliko hivyo; vinginevyo atatoa kafara ya mnyama aliye sawa na huyo aliyemuwinda au atatoa thamani yake anunue vibaba vya chakula kinacholiwa sana katika sehemu hiyo, na kumlisha kila maskini kwa vibaba vitakavyopatikana. Hivi ndivyo tunavyoagizwa katika Qur-an:


Enyi mlioamini! Msiue mawindo na hali ya kuwa mmo katika Hija au ‘Umra. Na miongoni mwenu atakayemuua makusudi basi malipo yake yatakuwa kwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wanaofugwa kama watavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu.Mnyama huyo apelekwe ilipo Ka ’aba (akachinjwe na kutolewa sadaqat huko) au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake (hili). Mw enyezi Mungu ameyafuta yaliyopita; lakini atakayefanya tena Mw enyezi Mungu atam uadhibu. Na Mw enyezi Mungu ndiye Mw enye Nguvu na Mwenye kuadhibu. (5:95).