3.
3. Tawaf
Kutufu ni kitendo cha kuizunguka Kaâaba mara saba kuanzia kwenye Jiwe Jeusi (Hajaratil-aswad). Wakati wa kuzunguka Kaâaba inakuwa upande wa kushoto, yaani mzunguko ni kinyume na ule wa saa (anti-clockwise). Kutufu ndio Ibadah ya kwanza anayoifanya mwenye kuhiji au kufanya âUmra mara tu baada ya kuizuru Kaâaba na kubusu Jiwe Jeusi.
Masharti ya Tawaf
Mwenye kutufu hana budi kuwa twahara. Yaani awe ameepukana na najisi na aina zote za hadath - asiwe na janaba, hedhi wala nifasi na awe na udhu.
Kwa wanawake wenye hedhi wanaruhusiwa kuingia katika Ihram na kufanya vitendo vyote vya Hija isipokuwa kutufu kama tunavyofahamishwa katika hadith ifuatavyo:
Amesimulia Aisha (r.a): Nilikuwa katika hedhi nilipoingia Makka, kwa hiyo sikuweza kutufu wala kusali. Kisha nilimfahamisha Mtume wa Allah, akaniambia, âfanya vitendo vyote vya Hija kama wengine lakini usitufu mpaka uwe twahara.: (Bukhari).
Namna ya Kutufu
Kama kawaida ya kila ibada, mwenye kutufu atatia nia ya kutufu na ataanza tawafu kwa kulibusu Jiwe Jeusi kisha atasema: âBismillaah Allaahu Akbarâ. Kama, kutokana na msongamano wa watu haitawezekana kulibusu âJiwe Jeusiâ, basi inatosha kwa kuligusa kwa mkono au kwa fimbo kisha kuubusu mkono au fimbo na kusema: âBismillaah Allahu Akbarâ. Kama vile vile itashindikana kuligusa jiwe jeusi kwa mkono au kwa fimbo, basi itatosha kuashiria kwa mbali kwa mkono au fimbo bila kubusu mkono au fimbo hiyo, kisha utasema: âBismillaah Allaahu Akbarâ. Hivi sasa kuna alama ya mstari mweupe uliochorwa ili kuwawezesha wale wanaozunguka mbali na Jiwe Jeusi kujua kuwa wamefika usawa na Jiwe Jeusi ili waashirie (Angalia kielelezo A na B uk. 297-8).
Wakati wa kuzunguka Kaâaba itakuwa upande wa kushoto na kuzunguka karibu na kuta za Kaâaba ni bora zaidi iwapo kuna uwezekano. Pembe nne za Kaâaba zimepewa majina. Pembe ya Mashariki ni hii yenye âJiwe Jeusiâ inaitwa Ar-Ruknul-aswad, ambapo mzunguko huanza baada ya kulibusu Jiwe Jeusi. Pembe inayofuatia wakati wa kuzunguka huitwa Ruknul-Iraaq, hii ni pembe ya Kaskazini, inayofuatia hii ni Ruknu-Sham, hii ni pembe ya Magharibi na inayofuatia ni Ruknul-Yaman, hii ni pembe
Ibn Abbas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: âKutufu katika Nyumba (Tukufu) ni kama mtu aliyeko kwenye swala isipokuwa mtu anaweza kuongea wakati wa kutufu. Kwa hiyo yeyote atakayeongea katika Tawaf hana budi kuongea maneno mazuri.â (Tirmidh, Nisai, Darimi).
Kwa wanaume ni sunnah kukimbia matiti (jogging or trotting) katika safari tatu za mwanzo, na kisha kumalizia safari nne zilizobakia kwa kutembea kawaida. Wanawake watatembea kama kawaida kwa mizunguko yote saba.Baada ya mzunguko wa saba, Haji au Hajjat ataendelea mbele mpaka pale aliposimama Nabii Ibrahim (a.s) wakati akiinua kuta za Kaâaba. Sehemu hii inaitwa âMaqamu Ibrahimâ ambapo alama ya unyayo wa Nabii Ibrahim (a.s) huonekana. Katika Qurâan tunakumbushwa juu ya alama hii.
Kwa yakini Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote. Humo mna is ha ra zilizo wazi (za kuonyesha utukufu wake na ukongwe wake. Miongoni mwa hizo ni) mahali alipokuwa akisimama Ibrahim, ...â (3:96-97).
Haji atakapofika âMaqamu Ibrahimâ ataswali rakaa mbili kwa kutekeleza amri ya Allah (s.w).
â... Na mahali alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kuswalia ...â (2:125).
Mtume (s.a.w) katika Hija ya kuaga alipofika hapa Maqamu Ibrahim alisoma kipande hiki cha aya kisha aliswali rakaa mbili. Katika rakaa ya kwanza alisoma: Suratul Kaafiruun na katika rakaa ya pili alisoma Suratul Ikhlas.
Kama kutokana na msongamano wa watu hapatakuwa na uwezekano wa kuswali karibu na sehemu hii, basi Hajj au Hajjat ataswalia sehemu yoyote katika usawa wa eneo hili la Maqamu Ibrahim.
Tawaf ya Mgonjwa au Mkongwe
Mgonjwa au mkongwe asiyeweza kutembea mwenyewe anaruhusiwa kutufu juu ya kipando kama vile mnyama au anaweza kubebwa katika machela au juu ya gari la kusukuma. Mtume (s.a.w) aliwahi kutufu juu ya mnyama alipokuwa ameumia mguu kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:
Amesimulia Ibn Abbas (r.a) kuwa Mtume wa Allah alitufu akiwa juu ya ngamia (wakati huo Mtume (s.a.w) alikuwa ameumia). Kila alipofika kwenye pembe ya Jiwe Jeusi aliiashiria kwa kitu mkononi mwake na kusema: âAllaahu Akbarâ (Bukhari).
Vile vile katika Hadith ifuatayo tunafahamishwa kuwa mtu anaweza kutufu akiwa amebebwa mgongoni:
Ames imulia Ummu Salama (r.a): âNilimfahamisha Mtume w a Allah juu ya maradhi yanguâ. Alisema: âTufu ukiwa umepanda juu ya migongo ya watu (ukiwa umebebwa) ...â (Bukhari).
Hukumu ya aliyekatisha Tawafu
Je, mtu akitokewa na dharura ikabidi akatishe tawafu kabla ya kumaliza mara zote saba, itabidi akirudi aanze upya? Kwa mfano mtu anaweza kutenguka udhu katikati ya tawafu ikabidi akatishe tawafu ili akatie udhu ndio arejee tena kutufu.Au, panaweza kukimiwa kwa swala ya faradh ikabidi akatishe tawafu ili ajiunge na jamaa kwa swala. Je, itabidi kuanza tawaf upya atakaporudi baada ya kutia udhu au baada ya kumaliza kuswali swala ya jamaa? Jibu la swali hili linajibiwa na Hadith ifu atayo:
âAtta (r.a) amesema: âKama mtu anatufu na pakakimiwa kwa ajili ya swala na swala ikaanza au kusukumwa na kutolewa nje ya sehemuâ alimokuwa, hana budi kurudi na kuanzia pale alipoachia (na kumalizia safari zilizobakia)â.
Hadithi hii pia imesimuliwa na Ibn Umar (r.a) na Abdur-Rahman bin Abuu Bakr (Bukhari).
Aina za Tawaf
(i)Tawaful-Quduum
Tawaf hii ni ile inayofanywa mara tu baada ya kuingia Makka kwa âUmra au kwa Hija. Katika tawaf hii Haji (mwanamume) atafunika bega lake la kushoto na kuacha wazi bega la kulia. Kitendo hiki kinaitwa âIztibaa.â Pia katika tawaf hii wanaume watakwenda matiti katika mizunguko mitatu ya kwanza. Kitendo hiki cha kukimbia matiti kinaitwa âRamalâ. Mizunguko minne iliyobakia itamaliziwa kwa kutembea kwa hatua fupi za kawaida.
(ii)Tawaful-Ifadha (Tawaf ya Nguzo)
Tawaf hii ni miongoni mwa matendo ya nguzo za Hija na hufanywa siku ya mwezi 10 Dhul-Hija baada ya kukamilisha ibada za Rami (kutupa mawe kwenye mnara mkubwa - Jamaratul-Aqaba), Nahar (kuchinja mnyama) na Halqa (kunyoa kichwa). âIztibaaâ na âRamalâ hazipo katika tawaf hii. Tawaf hii wakati mwingine inaitwa âTawafuz `Ziyaara.â
(iii)Tawaful-Widaa
Tawaf hii ya kuaga hufanywa wakati Haji akiwa tayari kuondoka Makka kurejea makwao. Hiki ni kitendo cha mwisho cha ibada ya Hija.
Umeionaje Makala hii.. ?
Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.
Soma Zaidi...