Ruhusa ya Ndoa ya Mke Zaidi ya Mmoja.

- Je, Ukeweza, (ndoa ya mke zaidi ya mmoja) humdhalilisha mwanamke?Jibu ndio:

- Kama ndoa hiyo imekusudiwa kumfanya mwanamke nguvu kazi ya uchumi, kuwa mwangalizi wa himaya ya mumewe tu, n.k.


- Kumzalia watoto wengi kama nguvu kazi ya uchumi, ulinzi wa mali yake tu, na kukosekana malengo ya ndoa, n.k.


- Kukosekana uadilifu na haki zake za msingi za kuolewa na kutekeleza majukumu yake ya msingi ili kufikia lengo kuumbwa kwake.


- Kunyanyaswa kama kupigwa, kutohurumiwa, kutukanwa, kutothaminiwa au kutengwa katika mahitaji ya kimaisha na kukidhi haja za kimwili pia.


Jibu hapana

- Kama ndoa inakusudiwa kumhifadhi na kumsitiri mwanamke na kila aina ya uovu na uchafu wa matamanio ya kimwili.


- Ikiwa ni kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwasitiri wajane walioachwa na waume wao bado wakihitaji malezi ya ndoa.


- Ikiwa ni kuwanusuru, kuwahifadhi na kuwasitiri wanawake wema waliokosa waume wa kuwaoa wasijejiingiza katika machafu.
Sababu ya kuruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja

Mafunzo ya Qur’an (57:25) na (4:3) yanatoa sababu zifuatazo;

i. Ukewenza ni ruhusa kutoka kwa Allah (s.w), hivyo wanaume hawana budi kuipokea kwa lengo la kumcha Allah (s.w).


ii. Ukewenza ni fursa pekee kwa wanaume waislamu wema, waadilifu kuwaoa wanawake hawa ili wasijekuolewa na wanaume waovu.


iii. Ukewenza hupelekea hifadhi kwa wajane, mayatima na wanawake wema wanaohitaji hifadhi, malezi, n.k.


iv. Ukewenza unaruhusika tu kwa kufanya uadilifu kwa wanawake wote katika kukidhi matamanio ya kimwili.
Hekima ya Ukewenza (kuoa mke zaidi ya mmoja)

Kuna sababu za kibinafsi, kimaadili, kiuchumi na kijamii kama ifuatavyo;

i. Kama mke ni tasa, hawezi kuzaa:

- Ikiwa mume anahitaji mtoto wa kumrithi kisheria na mkewe hawezi kuzaa hanabudi kuoa mke mwingine lakini akae kwa wema na wanawake wote.


ii. Kama mke ana maradhi ya kudumu:

- Kama mke ana ugonjwa wa kudumu na hawezi kumkidhia mahitaji ya kimwili, mume hanabudi kuoa mke mwingine na kuishi nao kwa wema.


iii. Kuwahifadhi Wanawake wajane na walioachika:

- Wanaume wanalazimika kuoa wake zaidi ya mmoja kama kuna wanawake wajane waliofiwa na waume zao au walioacha.


iv. Kuwapa hifadhi wanawake waliozidi idadi ya wanaume katika jamii:

- Kama wanawake watakuwa wengi katika jamii, italazimika wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja ili kuepusha kuenea machafu na maovu.


v. Kuwapa hifadhi na malezi watoto yatima:

- Mwanamke akifiwa na mume na ana watoto, malezi kamili hukosekana kama wazazi, hivyo kuolewa kunaboresha malezi kwa watoto walioachwa.