4. FAMILIA YA KIISLAMU

4.1. Ndoa Katika Uislamu

1. Maana ya Ndoa:

Kilugha: ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii.
Kisheria: ni mkataba wa hiari wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kuzingatia sharti na taratibu za Kiislamu.
2. Umuhimu wa ndoa katika Uislamu

Ni jambo lililokokotezwa sana kwani ni katika Sunnah za Mtume (s.a.w) yenye umuhimu ufuatao;
i. Kuhifadhi jamii na zinaa

- Ndoa hukinga wanandoa na jamii kwa ujumla na zinaa kwa kuhifadhi tupu zao na kukidhi matamanio baina yao.
Rejea Qur’an (5:5), (4:24)ii. Kuendeleza kizazi cha mwanaadamu kwa utaratibu mzuri

- Lengo la ndoa pia ni kuhifadhi, kutunza na kuendeleza kizazi cha mwanaadamu bila kuzaliana kiholela.
Rejea Qur’an (4:1), (42:11)iii. Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia

- Ndoa huleta utulivu katika moyo kati ya wanandoa na kupatikana huruma, mapenzi na ushirikiano baina yao
Rejea Qur’an (30:21), (2:187)
iv. Kukuza uhusiano na udugu katika jamii

- Uhusiano na udugu kati ya wanafamilia walioana huimarika na kuongezeka zaidi kuwa ukoo, kabila, taifa, n.k
Rejea Qur’an (25:54), (49:13)v. Kukilea kizazi katika maadili

- Ndoa inakusudiwa kuwa kiungo cha kulea na kuelimisha kizazi katika tabia na maadili mema anayoyaridhia Allah (s.w).


vi. Kumuendeleza mwanaadamu kiuchumi

- Ndoa huchochea wanandoa na wanajamii kwa ujumla kujijenga kiuchumi ili kukidhi mahitaji muhimu ya kimaisha na kibinaadamu.
Rejea Qur’an (6:151)