Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
MADHARA YA GONORIA (GONORRHEA) ENDAPO HAITATIBIWA
Endapo gonoria itachelewa kutibiwa inaweza kuleta madhaya mengi ndani ya mwili kuanzia ugumba, kudhoofu mwili, maumivu na mengineye. Yafuatayo ni madhara ya kuchelewa kutibu gonoria:-
1.Ugumba kwa wanawake. Ugonjwa huu kwa mwanamke unakula via vya uzazi kwa fujo sana. Unaathiri mirija ya falopia ambayo nduo inayohusika kubeba yai na utungaji mzima wa mimba na kusababisha PID yaani Pelvic Inflamatory Deseases. Hivyo mwanamke anahitajika atibiwe mapema kabla madhara hayajakuwa makubwa.
2.Ugumba kwa wanaume. Kwa wanaume gonoria huathiri vimirija vijidogo vilivyopo kwenye korodani. Mirija hii hujulikana kama epididymis. Hali hii hupelekea kuharibika kwa mirija hii hivyo kushindwa kubeba mbegu za kiume kuzitoa nje. Ugonjwa unaosababishwa na uharibifu huu hujullukana kama epididymitis.
3.Mashambukizi ya viungo vingine vya mwili na kuleta homa, upele, vidonda, maimivu ya viungo, kukaza na kuvimba kwa viungio.
4.Huongeza hatari zaidi kwa mwenye VVU na UKIMWI. Watu wenye VVU na UKIMWI ni rahisi kueneza gonoria kwenda kwa mwingine.
5.Kwa watoto waliop[ata gonoria wakati wa lujifunguwa wanaweza kupata upofu na madhara mengine kati afya zao.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yanayosababishwa na hali za maisha
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisukari Aina ya kwanza ambapo kwa kitaalamu huitwa Diabetes type 1, ni hali ambayo utokea ambapo mwili ushindwa kutengeneza insulini ambayo uweka sukari kwenye hali ya usawa.
Soma Zaidi...Utajifunza chanzo cha vidonda vya tumbo, dalili zake, dawa na matibabu yake pamoja na njia za kujilinda na vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa uti wa mgongo, ni ugonjwa unaoshambulia sehemu inayofunika ubongo na pia sehemu ya spinal cord
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Njia za kufanya Ili kupunguza maumivu ya tatizo la uti wa mgongo, ni njia unazopaswa kufanya pale unapokuwa na tatizo la uti wa Mgongo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini
Soma Zaidi...Post hii inahusu sababu za mtu kuwa na mfadhaiko na wasiwasi, mfadhaiko ni nguvu fulani anayoisikia ndani mwake kwa sababu ya tukio la kushutushwa linalomfanya afikilie sana,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza vitu vinavyosababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza maana ya homa ya ini. Pia utajifunza chanzo kinachosababisha homa ya ini. Makala hii itakuwa endelevu hivyo usikose muendelezo wake.
Soma Zaidi...