Menu



Madhara ya kutotibu uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo.

1. Maambukizi kwenye figo.

Kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo hali hii usababisha bakteria kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo na pengine maambukizi yanakuwa makubwa mno yanayopelekea kuaribika kwa figo na kumbuka figo ni kitu muhimu sana kwenye mwili kwa hiyo maambukizi yakiwa makubwa figo linakuwa kwenye hali ya hatari, kwa hiyo tunapaswa kutibu ugonjwa huu mapema Ili kuepuka kuepusha kuaribika kwa figo kwa sababu dawa hospitalin zipo na ugonjwa huu wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo unatibika kwa hiyo tutibu ugonjwa huu Ili kuepusha madhara mbalimbali.

 

2. Kuwepo na damu kwenye mkojo.

Kitendo Cha kuwepo kwa damu kwenye mkojo uonekana katika vipimo ,hii ni hali ya hatari kwa sababu maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo yanaonekana kuwa makubwa zaidi kwa sababu wadudu wameshakula sehemu mbalimbali na kusababisha mkojo kuwa na damu, kwa hiyo tunapaswa kuelimisha jamii kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huu na kuwa unatibika mtu yeyote akiona dalili ya damu kwenye mkojo anapaswa kwenda hospitalini kupima Ili kuweza kupata matibabu kwa kuwa watu wengi wameugua ugonjwa huu na wamepona.

 

3. Uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo umfanya mgonjwa ajisikie vibaya kwenye jamii.

Hii utokea pale mgonjwa mwenye tatizo hili akiwa kwenye jamii anakojoa damu, mkojo una harufu mbaya, anahisi maumivu akiwa kwenye jamii ambayo haieleweki watu wanaweza kumcheka na mgonjwa anaweza kujisikia vibaya na kuendelea kuwa na wasiwasi na kuishi bila raha kwenye jamii.kwa hiyo tutibu ugonjwa huu na tuwaone wagonjwa wa hivi kama watu wengine na kuwasaidia kwenda hospitalini Ili wapate huduma kwa kuwa ni ugonjwa unaweza kumpata kila mtu yeyote hakuna mwenye nao.

 

4. Maambukizi kwenye via vya uzazi.

Ugonjwa huu ikiingia kwenye kibofu Cha mkojo na baadae maambukizi yanaweza kusambaa mpaka kwenye via vya uzazi na yakishambulia uko yanaweza kuleta madhara makubwa zaidi kwa hiyo Tiba ni lazima, maambukizi yakizidi yanaweza kuleta hata na Kansa iwapo mgonjwa hakutibiwa mapema.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 1155

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Je mtu akapima ukimwi na kile kipimo kidogo .je kina usahihi au la ..na pia kama inaonyesha mistari miwili.

Hivi umeshawahi kuwazakuwa jekipimo cha HIV ni sahihi kwa kiasi gani. Unadhani huwa kinakoseaga kutoa majibu?

Soma Zaidi...
dalili za ukimwi huchukua muda gani?

Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.

Soma Zaidi...
Mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto

Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia katika makuzi ya mtoto, mtoto katika makuzi yake anahitaji kutunzwa vizuri Ili akue kwa afya nzuri bila magonjwa

Soma Zaidi...
Madhara ya ugonjwa wa ukimwi kwenye jamii.

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Sababu zinazopelekea maumivu ya Matiti.

 Maumivu ya matiti hutokea zaidi kwa watu ambao hawajamaliza hedhi, ingawa yanaweza kutokea baada ya kukoma hedhi. 

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa vitiligo, chanzo, dalili na matibabu yake

Katika post hii utajifunza kuhusu ugonjwa wa vitiligo, chanzo chake, dalili zake na matibabu yaje

Soma Zaidi...
Je wiki 1 dalili zinaonyesha za maambukizi ya ukimwi na wiki 3 vipimo vinaweza kuonyesha Kama umeasilika

Muda ambao maambukizi ya virusi vya ukimwi kuonyesha dalili unaweza kutofautiana kutika mtu hadi mwingine.

Soma Zaidi...
Kichwa kinaniuma mbele sielewi nini

Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa.

Soma Zaidi...
Dalili na ishara za anemia ya minyoo

Posti hii inshusiana na dalili za anemia ya minyoo

Soma Zaidi...