Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.
KUKUSANYIKA KATIKA DUA.
Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine. Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa.
Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao. Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin.
Amesimulia Habiib Ibn Salamah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia ‘aamiin’ isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo”. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "الدِّينُ النَّصِ?...
Soma Zaidi...Hizi ni Dua ambazo unatakiwa uziombe wakati wa shida na taabu
Soma Zaidi...