DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI.
Itambulike pia kuwa Allah huenda akacheewa kujibu dua ya mja wake si kwa sababu hataki ni kwa sababu anapenda kusikia sauti na maneno ya mja wake pindi anapoomba. Na hii ni kwa sababu Allah anapenda kuombwa. Pia wakati mwingine mtu anaweza kuomba dua na akajibiwa hapohapo au kwa haraka bila ya kujali awe muislamu ama sio muislamu. Hutokea kuwa Allah akawa hapendi sauti na maombi ya kafiri hivyo akaijibu dua ile ili amnyamazize mdomo wake.

Jambo la msingi ni kuwa Allah anapompenda mja anapenda pia kumsikiliza anayoyasema na anachokiomba. Na anapomchukia mja huwa hapendi hata kumuona akiomba hivyo humjibu ili anyamaze.

Amesimulia Jabir رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika (Malaika) Jibril ndiye aliyepewa kazi ya kutekeleza haja za wanaadamu, basi pindi mja kafiri anapoomba dua Allah husema kumwambia Jibril ‘ewe Jibril mpe haja yake kwani mimi sipendi kusikia dua yake. Na pindi anapoomba dua Mja muumini Allah humwambia Jibril ‘ewe Jibril izuie haja yake (usimjibu dua yake) kwani mimi napenda kusikia dua yake’”. )amepokea Ibn Najar).