Nafsi ya mwanaadamu

Nafsi ya mwanaadamu

Nafsi ya mwanaadamu


“Na katika ardhi zipo (alama namna kwa namna za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili. Na katika nafsi zenu (pia zimo ishara hizo)Je, hamuoni?” (51:20-21)
Ukimtafakari mwanaadamu utapata dalili nyingi zinazothibitisha kuwepo kwa Allah (s.w). Maeneo ya kutafakari ni pamoja na:



(i) Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu“Vipi mnamkanusha Allah (s.w) na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni, kisha atakufisheni, kisha atakurudisheni (tena) kisha kwake mtarejeshwa” (2:28)“Basi mbona (roho) ifikapo kooni, na nyinyi wakati ule mnamtazama. (56:83-84)Nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetoka roho) kuliko nyinyi, wala nyinyi hamuoni. (56:85)Kama nyinyi hamumo katika mamlaka (yangu), kwanini hamuirudishi (hiyo roho) ikiwa mnasema kweli?” (56:86-8 7).



(ii)Asili ya mwanaadamu “Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake) ni huku kukuumbeni kwa udongo kisha mnakuwa watu mnaoenea (kila mahali).” (30:20)



(iii)Kuumbwa Wanaume na Wanawake “Je! Anafikiri binaadamu kuwa ataachwa bure (asipewa amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je, hakuwa tone la manii lililotonwa? (75:36-37).Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha, kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.(75:38-39).Je! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?” (75:40). “Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya ziko alama (za kuwepo Allah) kwa watu wanaofikiri” (30:21)



(iv) Tofauti ya Lugha, Rangi, Makabila, Mataifa “Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake na uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi” (30:22). “Enyi w atu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kw a (yule) mw anamume (mmoja Adam) na (yule) mwanamke (mmoja Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mw enu mbele ya Allah ni yule amchaye Allah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Allah ni Mjuzi Mwenye habari (za mambo yote).” (49:13)



(v) Umbo na Sura “Ewe mwanaadamu! Nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamkanusha). Aliyekuumba na akakutengeneza, kisha akakulinganisha sawasawa. Katika sura yoyote aliyoipenda amekutengeneza ”. “Na katika umbo lenu na katika viumbe alivyovitawanya zimo alama kwa watu wenye yakini.” (45:4)



(vi)Chakula cha Mwanaadamu “Hebu mwanaadam na atazame chakula chake. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu (kutoka maw inguni).Tena tukaipasuapasua ardhi.Kisha Tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe. Na mizabibu na mboga. Na mizeituni na mitende.Na mabustani, (mashamba) yenye miti iliyosongamana barabara.Na matunda na malisho.Kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu. (80:24-32)



(vii)Ufanyaji kazi wa viungo vya ndani na nje ya mwili wa Mwanaadamu


“Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawasawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mw enyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo haki, lakini w atu w engi haw ajui.” (30:30) “Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na kuamka mchana na kutafuta fadhila Yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye kusikia.(30:23)
Mwanadamu japo analala kila siku, hajui chanzo cha usingizi. Mtu anapokuwa usingizini hajui chochote kinachoendelea, Je! ni nani anayeleta usingizi na kuuondoa?



(ix) Mwanadamu kumkumbuka Allah (s.w) wakati wa matatizo“Sema: Ni nani anayekuokoeni katika viza (taabu) vya bara na baharini? Mnamuomba kwa unyenyekevu na kwa sauti ndogo (mnasema): Kama akituokoa katika (baa) hii bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru (6:63)
Hata Fir’auni, aliyetakabari sana kiasi cha kudai kuwa yeye ni mkubwa kuliko Allah, alimkumbuka Mola wake pale alipokabiliwa barabara na matatizo.“Na tukawapitisha wana wa Israel katika bahari, na Firauni na majeshi yake wakawafuata kwa dhulma na jeuri. Hata kulipomfikia Fir’aun kuzama alisema, “Naamini kwamba hakuna aabudiw aye kwa haki ila yule wanayemuamini wana wa Israel na mimi ni miongoni mwa wanaotii”. (10:90)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1276

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Ni ipi maana ya Imani katika Uislamu, na ni zipi sifa za muumini.

Katika Uislamu imani inanguzo kuu 6.Pia muumini anatakiwa ajipambe na sifa za waumini. Posti hii itakufundisha kuhusu imani katika Uislamu.

Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida

Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?

Soma Zaidi...
Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku

Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.

Soma Zaidi...
KAZI ZA MALAIKA

Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.

Soma Zaidi...
Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)..

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...