image

MAAJABU NA UWEZO WA CHEETAH

5.

MAAJABU NA UWEZO WA CHEETAH

5.Cheetah

picHuyu ni katika wanyama jamii ya paka, na anafanana zaidi na mnyama anayeitwa puma. Cheetah ni mnyama mwindaji kama walivyo chui, simba na mbwa mwitu. Ijapokuwa cheetah wanafanana kwa sura na maumbile lakini unaweza kutofautisha mmoja kwa mwingine kwa kutofautisha rangi za kwenye mikia yao. Cheetah ni katika wanyama walio hatarini kwa kuuliwa kwani wapo wachache sana. Wataalamu wa wanyama na watafifi wanaeleza kuwa nchi ya Namibia ndio nchi pekee yenye cheetah wengi zaidi. Inakadiriwa cheetah wanaoishi maeneo haya wanafika 2500. Cheetah anaweza kufika uzito wa kilogramu 39 mpaka 65 (kg 29 - 65).

pic Tafiti zinaonesha kuwa cheetah ndiye mnyama anayekimbia kwa kasi zaidi kuliko wanyama wote wa porini. Cheetah anaweza kukimbia kwa mwendokasi wa kilomita 97 kwa lisaa (97 km/h) na anaweza kuendelea kukimbia kwa mwendokasi huu kwa umbali wa mita 300. Mwili wa cheetah hauna uwezo wa kutoa jasho hivyo anapokimbia kwa umbali huu wa mita 300 bila ya kukpata kiwindwa chake cheetah huachana nae kwa kuhofia mwili wake kupata joto ambalo linaweza kumpelekea kufa.

pic Wanyama hawa wanakaa kwenye makundi ya familia na mara nyingi madume wanapenda kupigana. Wanyama hawa wanapoteza asilimia 10 mpaka 13 ya vile walivyoviwinda kwa simba pamoja na fisi. Tafiti zinaonesha kuwa nusu ya mawindo yao wanafanikiwa kupata chakula. Cheetah ni katika wanyama waliop hatarini sana kwani wana windwa sana na binadamu kwa ajili ya kuuliwa. Mnyama huyu anapenda kuwinda kwenye maeneo yaliyo wazi pasiwe na miti mingia mabayo itamfanya akikose kiwindwa chake kwa urahisi.

Cheetah ni katika wanyama ambao wanaweza kuishi muda mrefu bila ya kunywa maji. Kwani anajipatia maji anayohitaji kutoka kwenye mwili wa kiwindwa chake. Pindi anapowinda humnyatio mnyama wake mpaka ukaribu wa mita 10 ndipo humkurupukia na kumkumbiza kwa mwendokasi wa zaidi sana, na hukata tamaa pindi akimkimbiza kwa umbali wa mita 300.


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 374


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

TUNAKUTAKIENI RANADHANI MUBARAKA
Wikibongo inawatakia waislamu wote heri ya mfungo wa ramadhaji Soma Zaidi...

Bezoa goat (mbuzi pori)
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sifa za mnyama bezoa goat (mbuzi pori) Soma Zaidi...

WELCOME TO OUR LIBRARY
Karibu sana Kwenye Maktaba Yetu Sasa umefika kwenye maktaba ya vitabu. Soma Zaidi...

More
Bila shaka umefurahishwa na huduma zetu, Je unataka huduma zaidi, Bofya kityfe cha Open hapo chini. Soma Zaidi...

OUR PRIVACY POLICIES.
Soma Zaidi...

Fast
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

YAJUWE MAAJABU YA MBUZI PORI
1. Soma Zaidi...

Home
Soma Zaidi...

MAAJABU NA NGUZU ZA TEMBO
TEMBO Tembo ni katika wanyama wa porini na ndiye mnyama mkubwa kuliko wote. Soma Zaidi...

MAKTABA YA VIBABU KUTOKA BONGOCLASS
Soma Zaidi...

Jifunze kupitia Bongoclass
Soma Zaidi...

Kitabu Cha ayansi ya viumbe
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...