Ujauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-
1.trimester ya kwanza (first trimester)
Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine ama moyo na masikio. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 85 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata hivyo wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.
Mabadiliko ya mwili katika kipindi hiki
A.Uchovu
B.Kukosa haja kubwa
C.Kichefuchefu
D.Maumivu ya kichwa
Nini hakitakiwi kufanyika katika kipindi hiki?
A.Wacha kuvuta sigara
B.Wacha kunywa pombe
C.Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktari
D.Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatarini
E.Punguza kuchwa chai kupitiliza
F.Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo
2.Trimester ya pili (second trimester)
Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza uonekana kwa ambaye anataka kuiona kwenye kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na nyinginezo.
Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu itarudi vyema na utawza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hki tumbo litaanza kuonekana kukuwa. Katika kipindi hiki jiepushe sana yafuatayo:-
A.Kuvaa nguo za kubana
B.Kuwa na hasira mara kwamara. Yaani jitahidi kkutafuta furaha, kaa na maafiki cheka na furahia.
C.Usikibane tumbo hata likiwa kubwa vipi.
Katika kipindi hiki unawezakuhisi kuingulia mra kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama ana mafua ama pua zimeziba ila akifina hakuna kitu. Pia anaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.
Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambuwa sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.
3.Trimester ya tatu (third trimester)
Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-
A.Anapima mkojo kuangalia protini
B.Atakuwa analkuangalia shinikizo la damu (presha)
C.Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtoto
D.Atakuwa akipima njia ya uzaziatakuwa acheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.
Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1284
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Changamoto za kwenye ndoa kwa waliotoa mimba mara Kwa mara
Posti hii inahusu zaidi changamoto za kwenye ndoa kwa wale waliotoa mimba mara Kwa mara,hizi ni changamoto za wakati wa kufanya tendo na mme wake au mtu mwingine kwa ajili ya kupata mtoto. Soma Zaidi...
Faida na hasara za kutumia kondomu kama njia ya uzazi wa mpango
Kondomu ni mpira ambao uwekwa kwenye uke au uume kwa ajili ya kuzuia mimba wakati wa kujamiiana Soma Zaidi...
dalili za mimba changa na siku ya kupata mimba
Jifunze namna ya kuthibitisha dalili za ujauzito kuwa ni za kweli. Tambuwa namna ya kupima mimba na muda mujarabu wa kupima Soma Zaidi...
Ni zipi njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukuletea njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume Soma Zaidi...
Dalili za ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi. Soma Zaidi...
Aina mbalimbali za mimba kutoka.
Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za mimba kutoka, hizi ni jinsi mimba inavyoonyesha dalili za kutoka na nyingine zinaweza kuonyesha dalili Ila kwa sababu ya huduma mbalimbali za kwanza hizo mimba zinaweza kudhibiiwa na mtoto akazaliwa. Soma Zaidi...
mambo ambayo utaulizwa mama mjamzito ukifika kituo cha afya unatakiwa utoe majibu sahihi.
Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Signs and symptoms of pregnancy.
In fact there is a lot of signs and symptoms of pregnancy a mother experiences throughout pregnant. These signs may start to be revealed immediately after conception or in the first week after conception. A term pregnancy is traditionally calculated by mi Soma Zaidi...
Dalili za mimba kutoka.
Post hii inahusu zaidi dalili za mimba kutoka, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mimba zote ambazo utaka kutoka kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Umuhimu wa kunyonyesha kwa Mama
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha kwa akina Mama, kunyonyesha ni kitendo ambacho Mama utumia maziwa yake na kumlisha mtoto pindi tu anapozaliwa mpaka wakati anapoachishwa titi, kunyonyesha huwa na faida kubwa kwa wote yaani Mama na mtoto, zif Soma Zaidi...
Dalili za kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi Dalili za Mama mwenye kifafa cha mimba, ili kifafa cha mimba kiweze kutokea lazima kuna dalili ambazo uweza kutokea kwa Mama kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji Soma Zaidi...