picha

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka


Hatua ya kwanza ilikuwa kuwahamishia Syria viongozi 10 wa upinzani kutoka Kufa. Wakorofi hawa walipopelekwa Syria, Amir Muawiya alizungumza nao na kusikiliza mafundisho yao lakini alipowasihi waache kupoteza watu walijifanya hawamuelewi kwa sababu hii Gavana Muawiya alimuandikia Khalifa Uthman kumuomba awarudishe walikotoka ili wasiwaharibu watu wa Syria kwa vile wanazungumza lugha ya shetani na lengo lao ni kuwagawa watu na kuunda fitna. Watu hawa walirudishwa Kufa na walipoendelea na shughuli zao walihamishiwa Hirus ambako walidhibitiwa kwa muda na gavana Abdur-Rahman mtoto wa Khalid.


Hatua ya pili iliyochukuliwa na Khalifa pamoja na Shura yake ni kutuma wajumbe wanne(4)kutembelea Dola nzima na kusikiliza malalamiko ya wananchi. Maswahaba waliotumwa ni Muhammad bin Muslimah, Usamah bin Zaid, Ammar bin Yasir na Abdullah bin Umar. Wajumbe hawa ambao walirudi watatu walitoa taarifa kuwa hakukua na malalamiko. Ammar bin Yasir alibakia Misr na kujiunga na wapinzani.


Kuwasilisha Malalamiko Kwenye Kikao cha Magavana


Kama kawaida magavana walikutana kila mwaka baada ya Hija. katika mwaka ule taarifa zilitolewa kuwa wenye malalamiko waende kuwasilisha malalamiko yao kwenye kikao hicho. Lakini hakuna aliyejitokeza. Si hivyo tu lakini Khalifa Uthman alitimiza dai la wapinzani hawa kwa kumuweka Gavana wanayemtaka Kufa. Walichokifanya wapinzani ni kuwa walikusanya kundi la watu wapatao elfu moja na kumzuia Gavana wa Kufa asirudi madarakani alipokwenda Madinah mkutanoni. Walimzuia mahali paitwapo Ajara, mtumishi wake aliuliwa na yeye akarudi Madinah. Khalifa akamthibitisha Abu Mussa kuwa gavana wa Kufa baada ya kutakiwa na wapinzani. Hapa Khalifa alionesha udhaifu, watu hawa walistahili kuadhibiwa kinyume na kukubali dai lao baada ya uhaini uliowazi.


Katika kikao cha Magavana Khalifa alitaka ushauri wa kuzima uasi nchini. Saad alishauri wapinzani wakamatwe na kuadhibiwa. Abu Sarah alishauri wasipewe posho; Ibn Aamir alitaka wapinzani wauawe; Muawiya pia alitaka zichukuliwe hatua kali. Kutokana na maoni haya Khalifa alijibu:


Ukatili sitoruhusu, kama mapinduzi yakija sitaki kulaumiwa. Ukianza hivi mwisho wake mbaya. Ingekuwa vyema pale mapema wakati uasi haujaenea. Sasa hakuna la kufanya ila kukaa kimya na kusubiri bila kumkosea mtu yeyote.


Muawiya alipokuwa anaondoka Madina alimsihi Khalifa akubali kuhama Madina lakini alikataa, na kusema hata kama ni kuokoa maisha yangu sitaondoka katika ardhi ambayo Mtume aliishi na kuzikwa.


Kisha Muawiya akamuomba akubali kuletewa jeshi lilinde mji wa Madina. Hali kadhalika Khalifa alikataa na kusema; “Sitawaweka askari wanaokaa karibu na nyumba ya Mtume”. Kwa hali hiyo Muawiya akajibu “Sioni kinachokusubiri ila umauti; “Mwenyezi Mungu ndie mlinzi wangu,” alisema Khalifa Uthman.38 ambaye alikuwa mzee wa miaka 82.


Uthman bin Affan, alijua hatari iliyokuwa inamkabili lakini hakutaka kutumia nguvu kuwaadhibu wapinzani wake kwa kuhofia kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe, alihiyari afe yeye kuliko kuzusha vita ambavyo vingegharimu roho nyingi.





                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 1191

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 ai web app     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Vita vya Al Fijar na sababu zake

Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.

Soma Zaidi...
Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Vitimbi vya Wapinzani Dhidi ya Ujumbe wa Nabii Shu’ayb(a.s)

Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.

Soma Zaidi...