Faida za kiafya za kula kabichi

  1. kabichi lina virutubisho kama protini, vitamini K, A, B6 na C. pia lina madini ya chuma, calcium na magnesium.
  2. Husaidia katika kupunguza mashambulizi ya mara kwa mara ya bakteria, virusi na fanasi
  3. Husaidia katika kupona kwa haraka kwa majeraha
  4. Husaidia kupunguza uharibifu wa seli dhidi ya kemikali mbaya
  5. Huboresha afya ya mifupa, misuli na mishipa ya damu
  6. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani
  7. Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kuzuia kukosa haja
  8. Hufanya moyo wako uwe katika afya njema
  9. Hushusha presha ya damu
  10. Hushusha kiwango cha cholesterol