Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya macho,dalili na matibabu yake
MARADHI YA MACHO
Matatizo ya macho yapo mengi katika jamii, lakini mara nyingi matatizo ya macho yanatibika iwapo mgonjwa ataonana na daktari mara atakapoona dalili. Miongoni mwa matatizo ya macho ni kupoteza uwezo wa kuona.
1.Kutoona karibu (long sightedness)Tatizo hili mara nyingi huwatokea watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.
DaliliA.Katika mazingira ya kawaida anaona sawa sawaB.Kushindwa kusoma herufi ndogo ndogoC.Kushindwa kufanya kazi za sehemu ndogo ndogo mfano kutunga sindano.
Matibabu: Kutumia miwani ya kusomea.
2.Kutoona Mbali (short sightedness)A.Hayana umri maalumB.Myopia – haoni mbali vizuriC.Hyperopia – haoni mbali na kichwa kinauma akikosa kuvaa miwani yenye namba ndogo kusaidia lense.
NB: Mgonjwa anasoma karibu bila miwaniMatibabu: Kutumia miwani ya kuonea mbali
3.Mtoto wa Jicho (cataract)DaliliA.Kidoto cheupe katikati ya kioo cheusi cha jicho (kinafunika mboni ya jicho)B.Kidoto cheupe kisichobadilika kwa mwangazaC.Kupunguza nuru ya macho
NB - Mtu anaweza kuzaliwa nacho au kupata ukubwani, inaweza kuwa kwenye jicho moja au yote. Mgonjwa huona mchanganyiko wa rangi anapoangalia mwangaza kama taa za umeme au gari.
MatibabuMtoto wa Jicho huwa anatibika kwa upasuaji mdogo na kumuwezesha mgonjwa kuona tena.
4.Presha ya macho (glaucoma)Tatizo hili husababishwa na kuongezeka presha ya jicho (intraocular pressure) kutokana na kukosekana uwiano wa mzunguko wa majimaji ndani ya jicho (aqueous fluid) kinachotoka kidogo kuliko kinachoingia.
MatokeoGlaucoma hukandamiza na kuuharibu mshipa wa fahamu ya jicho na kusababisha kupungua kwa nuru na baadae kupoteza nuru ya macho.
Matibabu: Kuonana na daktari kwa ushauri na dawa
5.Macho tongoHutokea ama kwa mtu mmoja mmoja, makundi au kwa msimu.
Sababu:Vimelea ambavyo huzaliwa kwenye sehemu za uchafu Wakati wa msimu huambukiza kwa kukosa elimu ya afya, kwa mfano kutokuosha mikono baada ya kuamkiana na mgonjwa mwenye maradhi haya au kutumia vifaa vya macho kwa zaidi ya mtu mmoja kama vile miwani.
DaliliA.Kuhisi kama kuna mchanga ndani ya jichoB.Kuvimba mifuniko ya macho bila kupoteza nuru.C.Macho kuwa mekundu sana (conjuctivitis)D.Kutoka tongo kila mara
MatibabuMgonjwa atumie dawa alizoandikiwa na daktari tu, kwani dawa za matone za macho ni nyingi na zina kazi tofauti.
6.Matatizo ya sehemu nyeusi ya jicho (cornea)Kuna matatizo manne makubwa1. Kovu - kidoto/kibaka cheupe2. Kidonda - kidoto kijivujivu3. Kuingiwa na kitu - kemikali,mdudu, vumbi n.k4. Kutoboka na kutoa maji.Indhari: hali ya pili mpaka ya nne zikitokea mgonjwa akimbizwehospital wakati jicho limefunikwa baada ya huduma ya kwanza
DaliliKOVU1.Haina maumivu2.Jicho haliwi jekundu3.Jicho halivimbi4.kupungua nuru jicho
KIDONDAA.Kinayo maumivuB.Jicho lililoathirika huwaC.jekunduD.Jicho kupunguka nuruE.Kuuma jicho kwenyeF.mwangazaG.Kutoka machoziH.Jicho kuvimba
Kidonda kinaweza kusababishwa na bakteria, fangas, ukosefu wa vitamin A au kwa kuumia mfano; kujichoma na kitu chenye ncha au kitu kigumu, kuingiwa na kitu jichoni, kuungua au kuingia kemikali jichon.
Indhari: Iwapo jicho litaumia lifunike jicho lisipate mwangaza kisha mpeleke mgonjwa hospitali.
7. Kemikali na kuunguaKama mgonjwa ameingia kemikali kama vile acid, alkali, saruji, chokaa mtie maji ya mchuruziko kwa takriban dakika 15 mfululizo na baadae mpeleke hospitali
8.Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana)
Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.
DaliliA.Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui)B.Macho kubadilika rangi (kahawia)C.Kutokwa na machozi mengi (sana)D.Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali
MatibabuKusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi.Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari
9.Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho
DALILIA.Kinundu kisichoumaB.Mara nyingi hupona wenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu.C.Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.
10.Uvimbe katika mfuniko wa jicho (cellulitis)
A.uvimbe kwenye mifuniko ya jichoB.inaweza kuzuwia jicho kucheza (kutembea tembea)C.mara nyingi hutokea baada ya kusambaa kwa maambukizoD.ya socket ya jicho kutoka pembezoni kwa saines (sinusitis) za puaE.husababisha kupoteza nuru za macho
Matibabu: Mpeleke mgonjwa kwa daktari wa masikio, pua na koo (ENT)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
NAMNA YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupata nafuu kutoka kwa maumivu ya kidonda cha tumbo ikiwa utafata taratibu za kiafya kama:- 1.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa kiungulia, kiungulia ni kitendo cha kupanda kwa gesi kutoka kwenye tumbo mpaka kwenye mdomo,hali uwasumbua wengi na kusababisha hali isiyo rafiki.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kansa, ni dalili ambazo utokea kwa mtu Mwenye tatizo la ugonjwa wa Kansa ingawa sio lazima dalili hizi kutokea tukadhani kuwa ni Kansa Ila zilizonyingi huwa ni kweli dalili za kansa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Hivi umeshawahi kuwazakuwa jekipimo cha HIV ni sahihi kwa kiasi gani. Unadhani huwa kinakoseaga kutoa majibu?
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo Uweza kujitokeza na kuona kwamba ni Dalili za miguu kufa ganzi, pengine utokea kwa watu wote na pengine huwa ni kwa ghafla
Soma Zaidi...