Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu kwa wanawake kabla ya kubeba mimba,Ni mambo ya kuzingatia ili mama akija kubeba mimba awe mzima kimwili, ki afya na kisaikolojia na hivyo hivyo Mtoto atakayezaliwa atakuwa salama.
Mambo muhimu ya kuzingatia kwa wanawake kabla ya kubeba mimba.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa kila mama anapaswa kujifungua mtoto salama kiafya, kiakili na kisaikolojia hili hayo yatimie ni lazima maandalizi ya mbali kuwepo yaani maandalizi kabla ya kubeba mimba kama tutakavyoona hapo chini.
2.kwanza kabisa historia ya Mama na baba wote inapaswa kujulikana kama wanatumia vileo vikali, wanavuta sigara na ni njia gani ya uzazi wa mpango wanayotumia au kama kuna Magonjwa ya kuridhi kwenye familia kama hayo yote yatajulikana ni vizuri kuwapa ushauri ni lini na wakati gani wanapaswa kukutana na kupata mtoto watajayemtaka wakiwa katika hali nzuri na kwa akili timamu
3.Pia Mama anapaswa kupima urefu, uzito, mapigo ya moyo, msukumo wa damu, joto la mwili,upumuaji kuangalia matiti yake kama yana aina yoyote ya uvimbe na kuangalia kama mama ana ugonjwa wowote ambao akibeba mimba unaweza kuleta madhara kwake na kwa mtoto
4. Kuangalia kama Mlay wa kizazi unaweza kufunga iwapo kama mimba ilitungwa na pia kuangalia kama kuna Maambukizi yoyote kwenye mlango wa kizazi hasa kansa ya mlango wa kizazi.
5. Kuangalia kama kuna aina yoyote ya Maambukizi hasa maambukizi ya Magonjwa ya a ngono kwa sababu mama akibeba mimba na magonjwa hayo mimba inaweza kutoka kwa hiyo Magonjwa haya kama yapo yatibiwe mara moja.
6. Pia mama anapaswa kupima wingi wa damu, group la damu, RH factor, maambukizi ya virus vya ukimwi, sukari, mkojo, antibodies na mambo mengine yote mawili na mama akikutwa na shida yoyote anaambiwa cha kufanya na akiona kubwa yuko salama anaweza kubeba mimba na mtoto natumaini atakuwa salama. Kwa hiyo akina Mama kabla ya kubeba mimba mnapaswa kufanya hivyo ili kupata watoto wenye afya njema.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Kama na wewe unasumbuliwa na hali ya kupitiliza siku zako post hii itakusaidia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tiba ya awali kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, tunaita tiba ya awali kwa sababu baada ya kupima na kugunduliwa kwamba una tatizo au changamoto ya PID ni vizuri kutumia tiba hiii baadae ndipo utumie dawa.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Je anapatwa maumivu Γ°ΕΈΛΒ makali wakati wa tendo la ndoa ama ukiwa katika hedhi? Soma makala hii hadi mwisho
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa Mama mwenye mimba, ni kipindi ambacho Mama uhitahi uangalizi wa karibu zaidi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutanuka kwa tezi dume, ni tatizo ambalo linawakumba wanaume wengi kwa wakati huu kwa sababu ya kuwepo kwa maaambukizi kwenye tezi ambayo Usababishwa na vitu mbalimbali kama tulivyoona.
Soma Zaidi...