1. VIRUSI VYA ZIKA (ZIKV)

Mnamo mwaka 2016 World Health Organization (WHO) iliitisha kikao cha dharura mnamo mwezi tarehe 1 mwezi wa pili mpaka tarehe 13 mwezi wa nne. katika kikao hiki ilitangazwa kuwa virusi vya ZIKA husambazwa na mbu aina ya Aedes aegypti.

 

Virusi vya zika husababisha kuzaliwa kwa watoto wasio wa kawaida kama vile watoto kuwa na vichwa vidogo ni athari ya virusi hivi. kwa sasa virusi hivi vimesambaa zaidi ya nchi 40 duniani. mbu hawa si kama wa malaria ambao hung'ata wakati wa usiku, mbu wanaobeba virusi wa zika wanang'ata wakati wa mchana.

 

miongoni mwa dalili za uwepo wa virusi hivi mwilini hufanana sana na dalili za malaria ijapo kuna utofauti kiasi. Dalili za uwepo wa virusi hivi ni kama:-

  1. homa
  2. mapele
  3. athari kwenye macho
  4. maumivu ya kichwa
  5. maumivu ya misuli na viungio

 

Dalili hizi hizi huanza kutokea baada ya siku 3 mpaka 12 baada ya kupata virusi hawa. Ila tafiti zinaonesha kuwa yapata asilimia 80% ya watu wenye virusi hivi hawaonyeshi dalili yeyote na hawajui kama wana virusi hivi. Tofauti na kuwa virusi hawa wanasambazwa na mbu lakini pia tafiti zinathibitisha kuwa ngono pia huweza kuambukiza virusi hivi.