image

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA, (homa,uchovu, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa n.k)

DALILI ZA MALARIA

 

Dalili za malaria huenda pia zikafungamana na maradhi mengine, lakini endapo zikikusanyika pamoja kwa asilimia kubwa vitakuwa vinaonyesha uwepo wa malaria. Kumbuka hizi ni dalili tu, lakini ni vyema kupima ili kuwa na uhakika zaidi kabla ya kumeza dawwa.

 

Homa, homa ni kupanda kwa joto mwilini. Kikawaida homa ni dalili za maradhi mengi sanaila leo nitakueleza homa ya malaria ilivyo. Kikawaida hima ya malaria inaweza kuambatana na mambo kadhaa wa kadhaa. Mambo hayo ni kama


Kuhisi baridi, kutetemeka na kutaka kuotea jua ama moto. Haijalishi ni saa ngapi iwe mchana ama usiku lakini mgonjwa atahisi baridi kali sana. Na inaweza kumsababishia hali ya kutetemeka viungo ama taya za mdomo wake kugongana kwa baridi. Hivyo endapo homa itaungana na hali hii huenda ni malaria. Lakini haitishi, inaweza pia kuambatana na japo hili hap chini:-

 

Maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli pamoja na viungio. Endapo homa ya mgojwa itaambatana na baridi, kisha ikafuatiwa na maumivu ya kichwa, maumivu haya yanaambatana na misuli kuuma pamoja na viungio. Mgonjwa anahisi katikati ya akutano ya viungio kama kuna vuta. Halli hizi zikikusanyika kwa pamoja huashiria malaria.

 

Mvurugiko wa tumbo unaopelekea kichefuchefu, ama kuharisha, ama kutapika ama vyote kwa pamoja. Mgonjwa anaweza kupata hali moja kati ya hizi ama akawa nazo zote. Mgonjwa anaweza kutapika maji ama chakula alichokula ama anaweza kutapika ile tunayoita nyongo. Hali hizi zinaweza kumpelekea mgonjwa akachoka sana. Tofauti na kuchoka huku lakini hatakuwa na hamu ya kula, na hata ladha ya chakula inabadilika na kuwa kichungu.

 

Uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya viungo, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutapika ama kuharishah. Hizi ni katika dalili za malaria.

 



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 761


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu. Soma Zaidi...

Dalili za anemia ya upungufu wa vitamin.
Anemia ya upungufu wa vitamini ni ukosefu wa seli nyekundu za damu zenye afya unaosababishwa na kiasi kidogo cha vitamini fulani kuliko kawaida. Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa hepatitis C
Hepatitis C ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoshambulia ini na kusababisha kuvimba. Watu wengi walioambukizwa na virusi vya Hepatitis C (HCV) hawana dalili. Kwa kweli, watu wengi hawajui kuwa wana maambukizi ya Hepatitis C hadi uharibifu wa ini Soma Zaidi...

Njia za kufanya ukiwa na tatizo la uti wa mgongo.
Posti hii inahusu zaidi Njia za kufanya Ili kupunguza maumivu ya tatizo la uti wa mgongo, ni njia unazopaswa kufanya pale unapokuwa na tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

Ni Nini husababisha kukosa choo? (Constipation)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo. Soma Zaidi...

NINI SABABU YA VIDONDA VYA TUMBO
NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo. Soma Zaidi...

Sababu za mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu.
Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuepuka minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuiepuka minyoo Soma Zaidi...

Madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye mifupa,ni madhara ambayo utokea endapo Maambukizi kwenye mifupa yasipotibiwa kwa mda wake. Soma Zaidi...

Aina za kisukari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za kisukari Soma Zaidi...

Matibabu ya vidonda sugu
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...

Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?
kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo. Soma Zaidi...