NAMNA YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEUNGUA
Kuungua kupo kwa aina nyingi. Mtu anaweza kuungua kwa umeme, moto wa kuni, moto wa gesi ama mvuke unaotoka kwenye mashine kama bomba la pikipiki. Pia mtu anaweza kuungua kutokana na miripuko kama baruti. Pia mtu anaweza kuunguwa kwa kemikali. Namna zote hizi zina utoaji huduma wake. Hapa nitaelezea kwa ufupi kuungua kwa moto.
Mtu anapoungua na moto angalia kwanza ni kwa kiasi gani ameungua. Kama ameungua sana ama eneo kubwa ni vyema kuwahi kutoa taarifa kituo cha afya kilicho karibu, ama kumuwahisha mgonjwa. Pia kuwa makini sana kama ameungua usoni, kwenye makalio ama miguu ama mikono au sehemu za siri.
Kama ameungua kawaida unaweza kumpatia huduma ya kwanza kisha uaendelea kumuangalia mgonjwa kama itahitajika kumpeleka kituo cha afya. Mtu aliyeungua unaweza kumpatia huduma ya kwanza kwa njia zifuatazo:
1.mwagilizia maji kwa muendelezo kwenye jeraha kwa muda wa dakika 15. ikishindikana kufanya hivi
2.Pepea sehemu yenye jeraha, ila usitumie barafu kwani linaweza kusababisha athari zaidi.
3.Unaweza kumpa mgonjwa dawa za maumivu kupunguza maumivu
4.Safisha jeraha kwa kimiminika cha iodine, ama aloevera gel. Na katu usimpake mafuta ya aina yeyote.
5.Unaweza kumpaka asali kwenye jeraha
6.ili kulinda jeraha dhidi ya kuvamiwa na bakteria mpake mmgonjwa kimiminika cha antibiotic
7.Lizibe jeraha kwa kulifunga na bendeji ama kitambaa kilicho safi na hakikisha hukazi sana wakati wa kufunga.
8.Angalia hali ya mgonjwa kisha umpeleke kituo cha afya kilicho karibu kwa uangalizi zaidi
2.. HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA (CARDIOPULMONARYRESUSCITATION) AU CPR
Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema. Ukikutana na mtu huyu usimkimbie. Kwanza msogelee karibu kisha hakikisha kama yupo hai ama laa. Kama yupo hai, kwanza angalia kama utaweza kupiga simu kituo cha afya, ama mtaalamu wa afya. Hakikisha maamuzi haya na utekelezwaji unafanyika haraka bila ya kuathiri hali ya mgojwa.
Baada ya kujiridhisha na maamuzi uliyochukuwa unaweza kuanza huduma ya kwanza, ya kumsaidia mgonjwa asiyepumua aweze kupumua. Hapa tutafanya huduma ya kwanza itambulikayo kama CPR. Hii ni huduma ya kwanza inayohitaji umkini wa hali ya juu. Lakini kwa ambaye hafahamu chochote kuna namna anavyotakiwa kufanya
1.mlaze mgonjwa kichalichali juu ya sehemu iliyo ngumu, isiwe sehemu inayobonyea kama kitandani
2.Punguza nguo zilizopo kifuani kwake, na kama ni mwanaume unaweza kumvua shati kabisa.
3.Bidua kidogo kichwa cake
4.Weke mkono wako wa mmoja juu ya mwengine, kisha iweka katikati ya chuchu za mgonjwa.
5.Anza kumbonyeza kifua chake kwa wastani wa mibonyezo 100 paka 120 kwa dakika moja. Yaani karibia mibonyezo miwili kwa dakika.
6.Hakikisha unabonyeza kwa nguvu mpaka uone kifua cha mgonjwa kinapanda na kuchuka kutokana na mibonyezo yako.
7.Usizidishe nguvu kupitiliza ukavunja mifupa ya mgonjwa.
8.Enelea kufanya hivi mpaka utakapoona mgonjwa anweza kupumua.
9.Muwahishe mgonjwa kituo cha afya baada ya kuanza kupumua.
3.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.
Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.
Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-
1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.
2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.
3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana
4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji
5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.
6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.
7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.
8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya.
4.HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ANAYETOKWA NA DAMU YA PUA
Kama mtu anatokwa na damu za pua, basi juwa kuwa anahitaji huduma ya kwanza. Kwanza msaidie mgonjwa kumtuliza, asipaniki. Kutokwa na damu puani kunaweza kutibika bila hata ya kuhitaji kwenda hospitali. Ila kwanza angalia hali aliyo mgonjwa na ni kwa kiasi gani damu inatoka, na ni kwasababu gani.
Baada ya kujiridhisha na hali ya mgonjwa unaweza kutoa taarifa kwa watu wa karibu ama kuwasiliana na kituo cha afya jirani. Wakati ukisubiri msaada unaweza kumpa mgojwa huduma ya kwanza kwa kufuata njia zifuatazo:-
1.mkalishe mgonjwa na ainamishe kichwa chake kwa mbele
2.Kwa kutumia vidole vyako minywa pua yake kuziba matundu ya pua zake
3.Fanya hivi kwa kuziba a kuachwa kwa muda wa dakika tano
4.Endelea mpaka uone damu imekata
5.Kama damu itaendelea kutoka kwa muda wa dakika 20 zaidi basi mpeleke mgonjwa kituo cha afya jirani.
5.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATA JOTO LA JUU ZAIDI (HEAT STROKE)
Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida. Joto linaweza kufika nyuzi 40 za sentigredi. Hali hii inaweza kupelekea kufa kwa viungo vya ndani kama ini, figo moyo na ubongo. Ukikutana na mgonjwa wa hali hii kwa hakika anahitaji huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo.
Endapo mgonjwa huyu hduma ya kwanza ikichelewa inaweza kuhatarisha maisha yake ama uharibifu wa afya yake kwa ujumla. Endapo hali hii itaambatana na homa kali, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutokwa n adamu za pua, ama kuchanganyikiwa mpeleke mgonjwa kituo cha afya. Huduma ya kwanza kwa mgonjwa huyu ni kama ifuatavyo:
1.mpunguzie mgonjwa nguo, abakiwe na nguo laini na chache
2.Mpeleke sehemu iliyopoa nabyenye baridi
3.Mpe maji yaliyopoa anywe
4.Tumia nguo mbichi na iliyopowa, ama sponji lenge maji yaliyopoa, fanya kama una mfuta mgonjwa.
5.Kama kuna feni karibu unaweza utumia ama muweke kwenye IC.
6.kama hali inaendelea basi awahishwe kituo cha afya mara moja.
6.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo
1.kichwa chake kipo katika pembe tatu
2.Rangi zake zinameremeta sana
3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka
4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu
Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-
1.Uchovu
2.Kizunguzungu
3.Anaweza kuzimia
4.Kichefuchefu
5.Kuharisha
6.Kutapika
7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi
8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa
9.Kuvimba eneo alipong’atwa.
Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-
1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.
2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.
3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.
4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto
5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.
6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.
Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu.
7. HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO
hii ni hali ghafla inayopelekea moyo kutofanya kazi vyema ama kukimama kabisa. Hali hii ikitokea inaweza kupelekea ukosefu wa hewa ya oksijeni mwilini na hatimaye kuanza kuathiri ubongo. Ukikutana na mtu wa namna hii utambue kuwa anahitaji msaada wa haraka sana.
Hakikisha unaomba msada wa kuwaishwa mgonjwa kituo cha afya. Mpunguzie nguo ili aweze kupata baridi. Muangalie vyema kama anaweza kupumua, kama hapumui ama anapata shida kupumua ana za kumfanyia huduma ya kwa nza ya CPR.
1.mlaze mgonjwa kichalichali juu ya sehemu iliyo ngumu, isiwe sehemu inayobonyea kama kitandani
2.Punguza nguo zilizopo kifuani kwake, na kama ni mwanaume unaweza kumvua shati kabisa.
3.Bidua kidogo kichwa cake
4.Weke mkono wako wa mmoja juu ya mwengine, kisha iweka katikati ya chuchu za mgonjwa.
5.Anza kumbonyeza kifua chake kwa wastani wa mibonyezo 100 paka 120 kwa dakika moja. Yaani karibia mibonyezo miwili kwa dakika.
6.Hakikisha unabonyeza kwa nguvu mpaka uone kifua cha mgonjwa kinapanda na kuchuka kutokana na mibonyezo yako.
7.Usizidishe nguvu kupitiliza ukavunja mifupa ya mgonjwa.
8.Enelea kufanya hivi mpaka utakapoona mgonjwa anweza kupumua.
9.Muwahishe mgonjwa kituo cha afya baada ya kuanza kupumua.
8.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEKUNYWA SUMU
Maisha ya mtu yanaweza kuwa hatarini ama kupotea mara moja baada ya kunywa sumu. Sumu inaweza kuwa katika vidonge, kimiminika, katika hali ya hewa ama kwenye sindano. Hapa nitazungumzia tu sumu inayoliwa na kuingia kwenye tumbo kwa njia ya mdomo. Sumu hii inawez akuwa ya panya am vidonge vya dawa.
Ukimuona mtu amekunywa ama kula sumu usimkimbie, na tambua kuwa anahitaji msaada wako. Kwanza angalia vyema hali yake na ukiwezekana ita msaada kwa haraka. Baad ya kufanya maamuzi kulingana na hali ya mgonwa unaweza kuanza kumpa huduma ya kwanza:
1.Mtapishe mgonjwa: kumtapisha mgonjwa ni katika njia nzuri na za haraka sana katika kupunguza athari za sumu. Unaweza kumtapisha mgonjwa kwa kumuingiza vidole mdomoni. Kama sumu ni ya kemikali mathalani amekunywa tindikali, njia ya kumtapisha sio njia sahihi.
2.Mpe maji mengi sana anywe. Kunywa maji mengi kutasaidia kupunguza makali ya sumu na kuiyeyusha kwenye maji.
3.Mpatie mgonjwa maziwa anywe. Unywaji wa maziwa uje baada ya kumtapisha. Usije mtapisha baada ya kumpa maziwa. Pia kama maziwa yapo usimpe maji mgonjwa.
4.Kama hali ya mgonjwa haijatengemaa, awahishe kituo cha afya kilicho karibu kwa haraka zaidi.
9.HUDUMA YA KWANZA KWA MWENYE KIZUNGUZUNGU
Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa. Kizunguzungu kinaweza kuwa ni dalili ya tatizo flani kwenye afya ya mtu. Maradhi mengi yanahusiana na kizunguzungu, hivyo baada ya huduma ya kwanza na mgonjwa akawa hajambo ni vyema aende kituo cha afya akajuwe chanzo cha kizunguzungu:
Mtu mwenye kizunguzungu anaweza kujipa huduma ya kwanza mwenyewe. Vinginevyo anaweza pia kupata maelekezo kutoka kwa mtu aliye karibu naye kwani siku zote mgonjwa anakosa uwezo wa kujimilikia\ hasa kujipa huduma ya kwanza.
1.Kwanza mwenye kizunguzungu anatakiwa akae chini
2.Kama alikuwa akitembea ama alikuwa akifanya shuhuli yeyote anatakiwa aache na akae chini kabisa na wala asichchumae.
3.Akaechini kipolepole na katu asiharakishe
4.Kama kukaa chini hakutoshi ni vyema alale, kama anaona kama dunia inazunguka asilale kichalichali.
5.Kama anakiu mpe maji ya kutosha anywe
6.Akae sehemu iliyotuia, isiyo na fujo wala mwanga mkali wa taa ama jua
7.Ni vyema kama atapata usingizi walau kidogo
8.Kizunguzungu kikiondoka kwanza akae chini kipolepole na anapotaka kusimama asimame kipolepole na katu asitumie kitu ili kimsaidie kusimama kama fimbo
11.HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUKWAMWA NA KUTU KOONI
Mtu aliyepaliwa ama kukwamwa na kitu kooni huwa anashindwa kuzungumza ama kupumua. Hali hii ikiendelea kwa muda inaweza kumsababishi amadhara makubwa hata kifo. Ubongo unaweza kufa ndani ya dakika chache sana kama ukikosa hewa ya oksijeni. Kama ukimkuta mtu amepaliwa ama kukamwa na kitu kooni na anashindwa kupumua unatakiwa umpe huduma ya kwanza:
Mtu anaweza kukwamwa ama kupaliwa na chakula, ama kitu kigumu kama kumeza pesa, jiwe barafu na kadhalika. Pia anaweza kupaliwa na maji, asali ama kimiminika chochote na kuzuia njia ya hewa. Hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Kama kupaliwa ni kwa kawaida amnapo mtu atakuwa na uwezo wa kukohoa, kulia, kuzungumza na kuhema, tambua kuwa anaweza kurudi katika hali ya kawaida hata bila ya kupata huduma ya kwanza. Ili kumsaidia mtu huyu kurudi haraka katika hali ya kawaida
1.Mwambie aendelee kuhohoa zaidi hii itasaidia kuondoa kilichokwama
2.Mwambe ajaribu kutema kicho kilichomkaba ama kilicho mkwama ama kusababisha kupaliwa
3.Katu usuthubutu kuingiza vidole vyeko kwenye koo lake eti kujaribu kukitoa kilicho mkaba
Kupaliwa kwa namna nyingine iliyo mbaya ni pale mtu anaposhindwa kusema, kukohoa, kulia ama kuhema. Bila ya huduma ya kwanza mtu huyu anaweza kuzimia na hatimaye kupoteza maisha. Huduma ya kwanza kwa mtu huyu ni:-
1.Muinamiche kifua chake kwa mbele, hii itasaidia kitu kilichomkaba kisiende ndani sana
2.Simama nyuma yake pembeni kidogo, weka mkono wako mmoja kwenye kifua chake na mgono wako mwingine anza kumpiga ngumi kwenye mgongo wake kati ya bega na bega, usawa na kifua kwa nyuma.
3.Angalia kama kilichomkaba kimeondoka
4.Kama hakijaondoka mpige tena kwa nguvu mapigo matano kama ni mtoto mminye kwa nguvu kwenye tumbo lake fanya hivi mara tano. Usifanye hivi kwa mtoto mdogo.
5.Kama hali inaendelea umpeleke kituo cha afya cha karibu.
12.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIKAZWA NA MISULI
Kukaza kwa misuli lunaweza kutokea muda wowote ila mara nyingi hutokea pindi mtu anapofanya mazoezi, amnapoogelea ama anapofanya kazi. Wakati mwingine misuli inaweza kukaza ukiwa umelala. Kama una tatizo hili hakikisha unakunywa maji ya kutosha muda wowote. Inaweza ikawa hatari zaidi kama misuli imekaza akiwa anaogelea, hapa anaweza kushindwa kuogelea na hatimaye kupoteza maisha.
Kukaza kwa misuli sio tatizo kubwa sana la kuathiri afya ya mtu ila linaweza kukuletea maumivu ya muda na baadaye kuondoka. Misuli inaweza kuachia yenyewe ama bada ya huduma ya kwanza. Mtu anaweza kujipa huduma ya kwanza mwenyewe ama kufanyiwa na mtu aliyepo karibu. Huduma ya kwanza kwa aliyebanwa na misuli ni kama:-
1.Mlaze chini ama miweke chini anyooshe miguu yake
2.Anza kuminyamninya kwa utaratibu misuli katika sehemu ulippokaza
3.Jribu kukunya na kukunjua kiungo husika kw autaratibu
4.Chua kwa utaratibu na maji ya moto ama tumia kitambaa kilichochovywa kwenye maji ya moto
5.Ama tumia barabu uliweke kwenye msuli uliokaza.
6.Baada ya muda hali hitakuwa sawa.
13.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Mara nyingi huwezi kujitambua kama unapresha hii ya kupanda mpaka pale inapotokea. Na ndio maana huitwa silent killer yaani muuwajiwa siri. Presha ya kupanda isipo tibiwa ama mgonjwa asipofata maelekezo vyema inaweza kusababisha shambulio lamoyo na kupalalaizi.
1.Muweke mgonjwa kwenye sehemu tulivu na iliyopowa
2.Mpunguzie nguo na abakiwe na ngue nyepesi na chache
3.Unaweza kumpepea ana muweke kwenye feni
4.Mpe vitunguu thaumu atafune, na afunge mdomo wakati anatafuna
5.Kama hali itaendelea mpeleke kituo cha afya kilicho karibu.
Presha ya kupanda isipotibiwa ama mgonjwa kufuata maelekezo vyema inaweza kusababisha athari kwenye moyo, kibofu na ubongo. Watu wengi wanakufa duniani kwa sababu ya presha ya kupanad. Wataalamu wa afya wametuwekea staili ambazo zinaendana na ugonjwa huu. Kama mgonjwa atafata maelekezo haya itamsaidia kuishi bila ya kupata presha ama tena kama ana presha itaweza kupunguza athari na isiwe inatoka mara kwa mara.
NJIA ZA KUKABILIANA NA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)
1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa dakika kama 30 mpaka 60. si lazima uwe unakimbia ama mazoezi magumu ya kutoa jasho, hapana unaweza hata kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo mrefu kwa lisaa limoja na ikawa ni mazoezi tosha.
2.Kula vyakula vilivyo bora kwa afya, ambavyo vinasaidia kupunguza ama kuzuia presha. Kitaalamu mlo huu huitwa DASH yaani Diet Aproaches to Stop Hypertension. Vyakula hivi ni kama:
A.Matunda
B.Mboga za majani
C.Nafaka nzima
D.Samaki, karanga na korosho
E.Wacha kula vyakula vyenye mafuta mengi
3.Punguza ulaji wa chumvi sana. Kuzidi kwa ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi kunaweza kusababisha presha ya kupanda. Kitaalamu ni kuwa ukila chumvi sana mwili unahitaji kupata maji mengi na hali hii itapelekea presha.
4.Punguza uzito uliozidi mwilini. Rafiki mkubwa wa presha ni kuzidi kwa uzito. Na tambuwa kuwa uzito wa mwili unatakiwa uendane na urefu wa mtu na si umri ama unene alio nao. hivyo tambua. Ili kuhakikisha kama uzito wako upo sawa unaeza kujipimia kiuno chako. Kikawaida wanaume wnatakiwa viuno vyao visizidi nchi 40 na wanawake viuno vyao visizidi nchi 35.
5.Punguza matumizi ya sigara ama wacha kabisa. Ndani ya sigara kuna kemikali za nicotine na nyinginezo. Nicotine ni rafiki sana na presha ya kupanda.
6.Punguza unywaji wa pombe ama wacha kabisa. Unywaji wa pombe sio hatari tu wa afya ya moyo lakini pia unaweza kuleta shida nyingine za kiafya kama saratani. Hakikisha kama ni mnywaji unapunguza unywaji ama unawacha kabisa itakuwa ni bora kwako.
7.Hakikisha huna misongo ya mawazo. Misongo ya mawazo inaweza kuwa ni adui mkubwa wa afya ya ubongo. Ni vyema kusamehe wanaokukosea na kuomba msamaha unapo kosea hali zote hizi mbili zitakusaidia kupunguza misongo ya mawazo. Jichanganye na watu na pemba kuwa mbali na fujo.
VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUPUNGUZA PRESHA YA KUPANDA AMA HULINDA MWILI DHIDI YA PRESHA YA KUPANDA.
Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-
Unaweza kupamana na presha kwa kufuata mashari kama kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni kama
1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni kama spinachi
2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo.
3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda.
4.Mayai
5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao.
6.Ulaji wa mbegu za mimea kama maboga na alizeti
7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna.
8.Makomamanga; unaweza kula atunda hili kama juisi ama kula kawaida.
RPESHA YA KUSHUKA (HYPOTENION)
Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Kama ilivyo presha ya kushuka presha ya kupanda unaweza kuizuia ana kujilinda nayo kwa kula vyakula salama.
VYAKULA MUJARABU KWA MWENYE PRESHA YA KUSHUKA
1.Tumia chumvi zaidi; wataalamu wa afya wanahimiza sana kutumia chumvi zaidi kwani madini ya sodium yaliyomo kwenye chumvi husaidia katika kupandisha presha. Ila tambua kuwa kwa wazee kuzidi kula chumvu kunaweza kusababisha moyo kujashinwa kufanya kazi vyema.
2.Kunywa maji mengi ya kutosha: maji husaidia katika kuongeza hali ya umajimaji kwenye miili. Hii husaidia kukabilia na upungufu wa maji mwilini (dehydration) hali hizi ni muhimu kwa kukabiliana na presha ya kushuka.
3.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kwa zaidi. Kwa mfano viazi mbatata, mchele na mikate
4.Kunywa chai yenye caffein;
DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA
1.Kushundwa kuona vyema
2.Kuchanganyikiwa
3.Kizunguzungu
4.Kuzimia
5.Uchovu wa hali ya juu.
6.Kuhisi baridi
7.Kushindwa kufikiri kwa kina
8.Kichefuchefu
9.Kushindwa kuhema vyema
10.Kutokwa na jasho
NJIA ZA KUKABILIANA NA MRESHA YA KUSHUKA
1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa muda wa dakika 30 mpka 60
2.Kunywa maji mengi na ya kutosha
3.Unapokaa usikae mkao wa kukunja miguu
4.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kama viazi mbatata, mchele na mikate
5.Punguza ama wach kabisa uvutaji wa sigara
6.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe.
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA
1.Lala chini kwenye kitu kilicho flati.
2.Kunywa maji mengi
3.Tumia chumvi, unaweza kuilamba unaweza pia kukoroga chumvi kwenye kikombe na kunywa.
4.Kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi ni vyema kuwasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe.
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI:
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo. Mara nyingi kwikwi huja na kuondoka yenyewe, lakini inaweza kuwa ni hali ya usumbufu ikiindelea kwa muda kadhaa. Kwa watoto kwikwi sio nzuri. Huduma ya kwanza kwa kwikwi unaweza kujifanyia mwenyewe ama kufanyiwa na mtu.
1.Kunywa glasi ya maji kwa haraka sana hakikisha umejaza glasi nzima
2.Mwambie mtu akutishe ama mtishe mtu mwenye kwikwi
3.Ufute ulimi wako nje
4.Ng’ata kipande cha limao
5.Kunywa maji kwa kutumia glasi ndefu
6.Tumia chumvi yenye harufu
7.Weka husu ya kijiko cha sukari nyuma ya ulimi wako.
8.Nyonza barafu
9.Kula asali ama sukari
10.Kunywa maji kipolepole
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA
Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte. Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya watu 10 mmoja anaweza kupata kifafa katika umri wake japo ni mara moja.mara nyingi kifafa ninatokea ndi ya muda mchache. Kikawaida ndani yasekunde kadhaa mpaka dakika 4 na hakizidi dakika 5.
Sio lazima kumpeleka mgonjwa hospitali ama kuhitaji msaada wa daktari. Kifafa kinaweza kuondoka chenyewe. Kumbuka hapa hatuzungumzii kifafa cha mimba. Taka msaada wa daktari ama mgonjwa apelekwe hospitali kama:
1.Hajawahi kuwa na kifafa toka azaliwe
2.Anashindwa kuhema ama kutembea baada ya kifafa kuondoka
3.Kifafa kimeendelea kwa muda zaidi ya dakika tano
4.Mtu amepata kifafa kingine punde tu baada ya kurejea hali ya kawaida kutoka kwenye kifafa
5.Mtu ameumia wakati alipopata kifafa
6.Kama kifafa kimetokea akiwa kwenye maji
7.Mtu ana magonjwa ya kisukari, maradhi ya moyo ama ana ujauzito
Ili kumsaidia aliyepata kifafa unaweza kumpa huduma ya kwanza kwa kutumia njia kama:-
A.Mlaze mgonjwa chini palipo safi
B.Mlaze mgonjwa upande mmoja
C.Safisha eneo alilopo mgonjwa hakikisha hakuna vitu vyenye ncha kali ama chochote cha kumdhuru
D.Weka kitu kilaini kwenye kicha chake kama mto ama nguo
E.Kama amevaa miwani ivue, vua na tai ana legeza
F.Kama kifafa kitaendelea zaidi ya dakika 5 mpeleke kituo cha afya kilicho karibu.
Usifanye haya kwa mtu aliyeanguka kifafa
1.Ukimkamate ama kumzuia miguu na mikono eti asihangaike
2. Usiweke chochote kwenye mdomo wake
3.Usijaribu kumfanyia CPR
4.Usimpe kitu chochote cha kula ama kunywa