tamaa

tamaa

33.

33. Kuepuka Tamaa na Kuombaomba



Kinyume cha kutosheka ni kuwa na tamaa au kutotosheka. Kutotosheka ni ufakiri wa moyo. Moyo wa kutotosheka huzaa tabia nyingi mbaya ikiwa ni pamoja na upupiaji mali, husuda, uchoyo, na kuomba omba. Muislamu anatakiwa ajitahidi kutosheka na alichonacho na hata kama anahisi yuko katika dhiki ajitahidi kujizuilia kunyoosha mkono wa kuomba chochote kwa yeyote kwa kadiri iwezekanavyo.
Tumekatazwa katika Qur-an kutamani vitu vya watu:


“Wala msitam ani vile am bavyo Mw enyezi Mungu am ew afadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma; na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile


w alivyovichuma;. Na mw ombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (4:32).
Kuhusu suala la omba omba Mtume (s.a.w) ametuusia katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule aombaye ili aongezee mali yake, haombi lingine ila moto wa maisha. (Muslim).
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Kama mmoja wenu ataomba bila ya sababu ya msingi atakutana na Allah na uso usiokuwa na nyama ”. (Bukhari na Muslim)



Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alipokuwa Mimbarini akitoa khutba juu ya kutoa sadaqa na kujizuia na kuomba omba alisema: “Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Mkono wa juu ni ule unaotoa na wa chini ni ule unaoomba”. (Bukhari na Muslim).
Kuomba kunaruhusiwa kwa dharura zifuatazo:



(i)Mtu aliyesimama kumdhamini mtu mwingine ili kuleta suluhu kati ya wagomvi wawili huyu anaruhusiwa kuomba hata akiwa tajiri. Kwa mnasaba huu, wadhamini wa Misikiti, madrasa, na shughuli mbali mbali za Kiislamu wanaruhusiwa kuomba michango ya Waislamu ili kufanikisha shughuli hizo.
(ii)Mtu aliyepata ajali na kuharibikiwa kabisa vitu vyote kama vile ajali ya moto, mafuriko, n.k.



(iii)Mtu ambaye amepigwa na ufukara na amekosa kabisa mahitaji muhimu ya maisha kama chakula, malazi na makazi. Lakini mtu akiwa kama na angalau chakula cha siku moja na malazi na akawa na dirham 50 mkononi mwake haruhusiwi kuomba kama tunavyofahamishwa katika Hadithi zifuatazo:



Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Anayeomba omba watu na ilhali ana mahitaji muhimu ya maisha atakuja siku ya Kiyama na kuomba omba kwake kama mikwaruzo, vidonda au majeraha usoni mwake. Iliulizwa: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni kiasi gani kinachomtosha mtu? Akajibu: Dirham 50 au thamani yake ya dhahabu (Abu Daud, Tirmidh, Nasai na Ibn Majah)



Sahl (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule anayeomba na ilihali anajitosheleza kw a mahitaji muhimu, anaomba


moto (Jahannam). Nufali (r.a) ambaye ni miongoni mwa wasimulizi wa hadithi hii katika sehemu nyingine aliuliza: Ni yupi mwenye uwezo ambaye kuomba ni haram? Akajibu Mtume (s.a.w): Yule mwenye uwezo wa kupata chakula cha asubuhi na usiku. Mahali pengine amesema: Yule mwenye chakula cha siku moja (Usiku na mchana). (Abu Daud).





                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 976

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 ai web app     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa

Hii post inahusu zaidi kazi za wahudumu wa afya wakati wa kutoa dawa, ni kanuni zinazopaswa kufuata wakati wa kutoa dawa kwa wagojwa.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyekazwa na misuli

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli

Soma Zaidi...
Kazi ya madini mwilini

Posti hii inakwenda kukueleza kuhusu kazi za madini mwilini

Soma Zaidi...
Jifunze jinsi ya kumsaidia mwenye kifafa

Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid

Soma Zaidi...
Hizi ni kazi za mapafu mwilini

Makala hii itakwenda kukufundisha kazi 5 za maafu mwilimi. Wengi tunajuwa tu kuwa mapafu yanafanya kazi ya kupumuwa. ila si hivyo tu yapo mengi zaidi.

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...