Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za VVU
DALILI ZA VVU
Dalilili za VVU huweza kutokea kuanzia wiki 2 mpaka 4 toka kuambukizwa. Lakini pia kwa baadhi ya ya watu inaweza kutokea mapema kabisa mnamo wiki ya kwanza. Na watu wengine dalili huizi zinaweza kutokea baadaye sana mpaka wiki ya sita. Dalili hizi si lazima mtu azipate zote. Dalili za mwanza zo VVU (HIV) ni pamoja na:-
Dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza
1.Homa
2.Kuhisi baridi ama kutetemeka
3.Uota upele
4.Kutokwa na jasho wakatio wa usiku
5.Maumivu ya misuli
6.Kupata vidonda vya koo, ama kuwasha kwa koo.
7.Uchovu mkali usio elezeka
8.Kuvimba kwa tezi node za lymph yaani kuvimba tezi za mtoki mapajani, kwapa na shingoni.
9.Kupata vidonda kwenye mdomo
Dalili za VVU katika hatuwa ya pili
Baada ya dalili za awali katika hatuwa ya kwanza hadi kufikia wiki ya sita dalili za awali zitapotea. Kisha mtu ataingia katika hatuwa ya 2. hatuwa hii hujulikana kama clinical latency Stage ama pia huitwa chronic HIV infections. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10 toka kuambukizwa.
Watu waliokuwepo katika hatuwa hii hawana dalili yeyote ile. Kama mtu atatumia ART anaweza kudumu katika hatuwa hii kwa makumi ya miaka, ila kwa ambao hawajaanza kutumia ART wanaweza kupita kwa haraka kwenye hatuwa hii. Katika wakati huu mfumo wa kinga unaendelea kuharibiwa, ila uharibifu utakuwa mdogo ama hakuna endapo mtu ataanza kutumia ART au ARV.
HATUWA YA MWISHO NI UKIMWI
Ikitokea muathirika hakutimia ART basi virusi vitaendelea kuathiri mwili wake na kumaliza seli za CD4. hizi ndizo seli za kinga ya mwili yaani zinalinda mwili dhidi ya mashambulizi ya vijidudu kama virusi, bakteria, fangasi na vinginevyo. Mtu wa kawaida ana seli za cd4 kuanzia 500 mpaka 1500 katika kipimo kimoja. Sasa zikishuka mapaka kufikia 200 mgonjwa huyu ataambiwa ana Upungufu wa kinga Mwilini yaani UKIMWI. Mtu huyu atakuwa na dalili zifuatazo:-
Dalili za Ukiwmi:-
1.Kupunguwa uzito kwa haraka bila ya sababu maalumu ijulikanayo
2.Kupata homa kali za mara kwa mara na kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku.
3.Kuchovu mkali sana usiojulikana sababu.
4.Kuendelea kuvimba kwa tezi za mtoki, kwapa na shingo
5.Kuharisha kunakoendelea zaidi ya wiki moja
6.Kutokwa na vidonda kwenye mdomo, ulimi, mkundu na sehemu za siri.
7.Kubana kwa pumzi
8.Kupoteza kumbukumbu, kukasirika mara kwa mara, ama kupoteza uwezo wa kuthibiti akili (kuchanganyikiwa)
9.Kuota mapele, majipu, mabumbuza kwenye ngozi, kope, pua na mdomoni
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi Ugonjwa wa ukoma ni Ugonjwa unaosababishwa na bacteria anayejulika kama mycobacterium leprae.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kuzungumzia ugonjwa wa gout unaosababishwa na ongezeko la asidi mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalilili za kukosa oksijeni ambalo kitaalamu hujulikana Kama apnea.kukosa oksijeni ni tatizo ambapo kupumua kwako hukoma na kuanza unapolala.
Soma Zaidi...MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu.
Soma Zaidi...Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ukimwi za kwenye ulimi na mdomo
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi adhari za ugonjwa wa Homa ya inni, hizi ni athari ambazo zinaweza kutokea ikiwa ugonjwa huu wa inni haujatibiwa, zifuatazo ni athari za ugonjwa wa inni
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa ambao husababisha kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Ambao kitaalamu hujulikana Kama Behcet .
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye nephroni, ni njia zinazotumika kuzuia maambukizi kwenye nephroni
Soma Zaidi...