image

Mafunzo ya DATABASE - MySQL somo la 7

Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.

SOMO LA SABA

Katika somo lililotangaulia tumejifunza namna ya kutengeneza table. Sasa katika somo hili tutajifunza jinsi ya kuedit jina la table, kufuta. Tutafanya haya kwa kutumia MySQL na kwa kutumia SQL command. Kabla hujaanza somo hili tengeneza table nyingine kisha iite text. Table hiyo ndio tunakwenda kuifanyia mazoezi ya kuiedit jina na kuifuta. Fuata maelekezo ya somo lililotangulia kutengeneza table.

 

Jinsi ya kubadili jina la table kwenye MySQL

Tunabadili jina kwa sababu maalumy, huwenda jina la mwanzo ni gumu sana ama haliendani na data ambazo zipo kwenye database. Ama linafanana na table nyingine ambayo unataka kuitengeneza. Ili kufanya hivi yaani kubadili jina fuata hatuwa zifuatazo:-

Tengeneza Table kwa kutumia command hii

CREATE TABLE IF NOT EXISTS test (

    id INT,

    name VARCHAR (255),

    aka VARCHAR (255)

    )

    

  1. Bofya hiyo table itafunguka utaona hizo column ambazo umetengeneza.
  2. Ingia kwenye operations
  3. Kwenda chini hadi ukute palipoandika table options
  4. Chini utaona palipoandikwa Rename table to na mbele yake kuna kabox.
  5. Kwenye kabox hako weka jina unalotaka lisomeke kwenye table yako mfano tutumie jaribio, hivyo futa jina la mwanzo kisha weka jaribio hapo
  6. Bofya GO
  7. Mpaka kufika hapo jina la table yako litakuwa limebadilika kuwa jaribio

 

 

1. Kubadili jina la table kwa kutumia SQL command

Sasa kama huhitaji kutumia MySQL interface kufanya hivyo unaweza kutumia SQL fuata hatuwa zifuatazo:-

 

        1. Funguwa uwanja wa SQL

  1. Kubadili jina tunatumia RENAME TABLE  au ALTER TABLE kisha inafatiwa na jina la mwanzo ambalo ni jaribio kisha unaandika to kisha unaweka jina jipya mfano test. Statement hii itakuwa hivi
  2. RENAME TABLE jaribio to test;
  3. Pia unaweza kutumia hii kubadili jina ALTER TABLE test RENAME to jaribio
  4. Baada ya hapo bofya GO
  5. Kufikia hapo utakuwa umebadili jina la table yako.

 

2. Kubadili jina la column

Chukulia unataka kubadili jina la column lmfano katika katika table hiyo tuliotoka kuirename ina column tatui mabzo ni id, name na aka. Sasa tunataka kubadili name tuweke firstname badala ya kuwa nme. Kufanya hivi kwa kutumia MySQL fuata hatuw zifuatazo:-

 

  1. Bofya hiyo table
  2. Bofya palipoandika structure
  3. Utaona column zote tatu zipo hapo
  4. Kwa upande wa kulia kwa kila column kuna palipoandikwa change. Bofya hapo
  5. Kutakuja ukurasa wenye vijibox vingi
  6. Tafuta kibox kilichoanikwa name
  7. Futa name kisha andika jina unalotaka kubadili mfano firstname kumbuka hakuna kuruka nafasi katika kuandika majina.
  8. Bofya neno save lipo upande wa kulia
  9. Mpaka kufika hapo utakuwa umeweza kubadili jina la column.

 

3. Kubadili jina la column kwa kutumia SQL

Tofauti na kupitia hatuwa hizo nyingi kwa kutumia SQL unaweza kubadili kwa haraka zaidi. Kufanya hivo fata hatuwa zifuatazo:-

  1. Ingia kwenye uwanja wa SQL
  2. Kubadili jina tunatumia ALTER TABLE kisha inafata jina la table unalotaka kubadili kisha unaandika neno CHANGE kisha unafata column unayotaka kubadili  halafu unafata kuweka jina ambalo unataka iwe, kisha utamaliza na kuandika type yake ya data kisha utaweka na character length yake iwe ndani ya mabao. Mfano wa statement hi kama hii
  3. Katika table yako ya jaribio kuna column inaitwa aka sasa tunakwenda kuibadilisha kuwa nickname.
  4. ALTER TABLE jaribio CHANGE aka nickname VARCHAR(255);

 

 

4. Kuongeza column kwenye table

Sasa kuna jambo hili. Baada ya kutengeneza table kumbe ukahitaji kuongeza column. Let say kwa mfano katika table yetu ya jaribio kuna column tunataka kuiongeza kwa ajili ya kkuweka namba za simu. Na tunataka kuiita phone. Kufanya hivi fata hatuwa zifuatazo kwa kutumia MySQL:-

  1. Bofya hiyo table yako.
  2. Bofya structure
  3. Shuka chini tafuta palipoandikwa Add utaona kulia kuna kabox ndani kuna namba moja. Hapo utaamuwa je unataka kuongeza column ngapi kama ni mbili utaweka mbili. Ok kwa saa wacha hiyo moja
  4. Kisha bofya GO
  5. Ukurasa mpya utafunguka na hapo utatakiwa kujaza taarifa kama ulivyojifunza kwenye somo la sita.
  6. Kwenye jina utaweka phone, kwenye type utaweka INT kwani type ya data hapa ni namba, kwenye length weka 15
  7. Bofya save
  8. Mpaka kufika hapo table yako ya jaribio itakuwa na column nne ambapo hii ya phone imeongezeka.

 

 

5. Kuongeza column kwa kutumia SQL

Sasa tunakwenda kuongeza column nyingine ambayo tutaiita jinsia. Tutakwenda kutumia SQL kufanya haya. Hivyo baada ya hapa table yetu itakuwa na column 5. fata hatuwa zifuatazo:-

  1. Funguwa uwanja wa SQL
  2. Kuongeza column tunatumia ALTER TABLE kisha jina la table kisha ADD kisha column unayotaka kuongeza kisha type of data ilifuataiwa na character length kwenye mabano. Kisha utatakiwa kusema kuwa column hiyo itakuwa baada ya column ipi. Hapa utatumia after. Kwa mfano katika mfano wetu itakuwa after nickname Kisha alama ya ; hivyo statement hii itaonekana hivi
  3. ALTER TABLE jaribio ADD jinsia INT(15) AFTER nickname;
  4. Bofya GO
  5. Mpaka kufuka hapa utakuwa umeongeza column nyingine ya tano.

 

 

6. Kufuta column kwa kutumia MySQL

Sasa unataka kufuta moja ya colun baada ya kuona haina kazi. Kufanya hivi ni rahisi sana . fanya hivi:-

  1. Bofya table
  2. Bofya structure
  3. Utaona column zote
  4. Kulia mwa kila column kuna neno limeandikwa Drop
  5. Bofya hilo neno kulia mwa column unayotaka kuifuta kwa mfano bofya hapo kwenye nickname
  6. Kabox ka alert katakuja kuuliza kuwa je unataka kufuta kweli. Wewe piga Ok
  7. Mpaka kufikia hapo utakuwa umefuta column hiyo.

 

 

7. Kufuta column kwa kutumia SQL

Kufuta column kw akutumia SQL. Kufanya hivi kwa command za SQL fuata hatuwa hizi:-

  1. Ingia kwenye uwanja wa SQL
  2. Kufanya hivi tutatumia ALTER TABLE kija litafuata jina la table ambalo ni jaribio. Sasa tunakwenda kufuta column ya phone. Hivyo baada ya kuandika jina la table andika neno DROP likifuatiwa na column ambayo unataka kuifuta ambayo ni phone kisha maliza na alama ya ; hivyo itasomeka hivi
  3. ALTER TABLE jaribio DROP phone;
  4. Bofya GO
  5. Utatakiwa kuthibitisha weka OK
  6. Mpaka kufika hapo utakuwa umeifuta colunm ya phone.

 

 

Tukutane somo la nane tutakapojifunz ajinasi ya kuweka data kwenye database. Hakikisha kablya ya kuingia somo la nane somo la sita umelielewa vyema vinginevyo utasumbuka.

 

 

Mafunzo haya yamekujia kwa ihsani ya Bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email: mafunzo@bongoclass.com

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tehama Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1053


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 5 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
katika somo hili la tano kwenye mafunzo ya HTML level 1 utajifunza jinsi ya 1.Kuweka picha 2.Kuweka rangi 3.Kuweka linki 4.Kupangilia position na alignment ya maandishi 5.Kuongeza ukubwa wa herufi 6.Kukoment Soma Zaidi...

Mafunzo ya Database MySQL DATABASE somo la 2
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 1 somo la 2 for beginner (html full course for beginners)
Somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2. Katika somo hili utajifunza maana ya HTML pamoja na historia yake fupi. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 8 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 8)
Hili ni somo la mwisho mafunzo ya HTML level 2 (html full course for beginners) Soma Zaidi...

Mafunzo ya database MySQL somo la 3
Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 1 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 4 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia. Soma Zaidi...

PHP level 1 somo la kumi (10)
Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement. Soma Zaidi...

Mafunzo ya DATABASE - MySQL database somo la 8
Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML Level 2 somo la 7 (HTML FULL COURSE FOR BEGINNERS LESSON 7)
Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi. Soma Zaidi...

Mafunzo yz database MySQL database somo la 12 (final)
Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database Soma Zaidi...