PHP LEVEL 1 SOMO LA KUMI NA MBILI (12) FINAL


image


Mafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya.


PROJECT KULINGANA NA COURSE HII.

Kama ulivyokwiisha kutambuwa kuwa katika kila baada ya kumaliza course tunaleta poject. Project hizi zitakusaidia mshiriki wa mafunzo haya kuweza kuelewa zaidi na kufanyia kazi kile ambacho kime fundhishwa. Hapa nitakuletea project tano ambazo ni:-

 

1. Kikokotoo cha hesabu (Simple calculator with php and html)

2. Kikokotoo cha umri (age calculator with php)

3. Code playground (HTML, CSS and JAVASCRIPT code playground with php)

4. Dodoso la usajili (databaseless registration form).

5. Kuhesabu idadi ya maneno kwenye sentensi ama paragraph

 

Project hizi ni program fupifupi ambazo zina msingi mzuri kwa mwenye kuanza. Uzuri wa project hizi zote ni za level ya chini ssana kiasi kwamba kama ulishiriki kwenye mafunzo yetu hazitakushinda. Kama ukipata ugumu tafadhali rudia somo lililotangulia la 11 katika mafunzo haya.

 

1. KIKOKOTOO CHA HESABU

Program hii itakuwa inafanya kaz ka ma kikokotozi yaani calculator. Yenyewe itahusika na matendo manne ya hesabu yaani kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Mtumiaji atahitajika kuingiza namba, tendo (+, *, - au /) kisha ataingiza namba nyingine, atabofya submit kisha atapata majibu.

 

Program itakusanya data zake kwa kutumia HTML form kisha itatuma namba atakazoingiza mtu kwenye variable za php. Kwa kutumia switch case utaweza kuchaguw tendo. Tafadhali pitia somo la 10 kwenye mafunzo haya upate kujifunza zaidi kama hujaelewa kuhusu switch case.

CODE ZA PROGRAM

<html>
<form method="post" action="">
<label>KIKOKOTOZI:</label><br>
    <input type="number" name="a" placeholder="0"><br>
    <input type="text" name="b" placeholder=""><br>
    <input type="number" name="c" placeholder="0"><br>
    <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a=$_POST['a'];
$b=$_POST['b'];
$c=$_POST['c'];
$result = "";





switch ($b) {
    case "+":
        $result = $a + $c;
        break;
    case "-":
        $result = $a - $c;
        break;
    case "*":
        $result = $a * $c;
        break;
    case "/":
        $result = $a / $c;
}
?>
<p>
    <input readonly="readonly" name="result" value="<?php echo $result; ?>">
</p>

 

2. DODOSO LA USAJILI

Katika program hii mtumiaji ataweza taarifa zake kisha zitakuja kama alivyoziweka. Program hii itakusaidia utakapokuja kujifunza namna ya kudisplay taarifa kutoka kwenye database. Kwa sasa hatutatumia database ila somo litakalofata taarifa hizi moja kwa moja zitatola kwenye database baada ya mtu kujiajili.

 

Program hii itatumia mafaili mawili. Moja ni la HTML kwa ajili ya kukusanya madodoso. Kisha faili lingine litakuwa ni kwa ajili ya kudisplay taarifa zilizojazwa. Katika faili la HTML kwenye action utakuta kuna link ya faili linalofata ambalo ndilo litakalopelekewa taarifa zilizojazwa kwa ajili ya kuchakatwa.

 

Ijapokuwa unaweza kuchanganya mafaili haya sehemu moja ;akini nimependelea kuyatengenisha kwa ajili ya kujifunza zaidi. Hivyo kama ndio na wewe unaanza weka mafaili mawili. Kisha faili m,oja ni la htm;l code na la pili ni kwa ajili ya php code.

 

Katika program hii faili la kwanza nimeliita p2.php ambalo litabeba php code na la pili p.php ambalo litabeba hyml code

 CODE ZA PROGRAM

p.php

<html>
<form method="post" action="p2.php">
<label>Sensa ya watu na makazi</label><br>
    <input type="text" name="a" placeholder="Weka jina lako hapa"><br>
    <input type="text" name="b" placeholder="Umri"><br>
    <input type="text" name="c" placeholder="Jinsia"><br>
    <input type="text" name="d" placeholder="Unapoishi"><br>
    <input type="text" name="e" placeholder="Hali ya ndoa"><br>
    <input type="text" name="f" placeholder="Elimu"><br>
    <br><br><input type="submit">
</form></html>

 

p2.php

<?php

$a=$_POST['a'];
$b=$_POST['b'];
$c=$_POST['c'];
$d=$_POST['d'];
$e=$_POST['e'];
$f=$_POST['f'];
$t = date("Y/m/d/l");
echo "<p>Karibu sana  <b>$a</b></p> <br><br> <u><b>Na hizi ndio Taarifa zako ulizojaza kwenye Sensa hii:-</b></u><br>";
echo "Jina: $a <br>";
echo "Umri: $b <br>";
echo "Jinsia: $c <br>";
echo "Unapoishi $d <br>";
echo "Hali ya Ndoa: $e <br>";
echo "Elimu: $f <br>";
echo "Siku ya kuandikishwa: $t"

?>

 

3. KIKOKOTOZI CHA UMRI

Katika program hii mtumiaji atatakiwa kuwka mwaka wake aliozaliwa kisha program itamtajia idadi ya miaka yake. Program imetengenezwa kwa kutumia kwaka 2021. yaani mtu akiingiza mwaka aliozaliwa program itachukuwa mwaka 2021 kisha itatoa huo mwaka na kupata miaka ya hiyo mtu.

 

Kwa mfano mtu akiingiza mwaka 2000 program itafanya 2021 - 200  = 21 hivyo idadi ya miaka ni 21. unaweza kimodify program hii kwa kutumia function date() ili iweze kuendana na muda, yaani itakuwa inachukuwa muda wa sasa. Mfano ifikapo 2022 program hii haitasema ukweli lakini kwa kutumia function date() haina aja ya kubadili 2021 kuweka 2022

 CODE ZA PROGRAM

<html>
<form method="post" action="">
<label>KIKOKOTOZI CHA UMRI:</label><br>
    <br><br>
    <label>Weka mwaka uliozaliwa</label><br>
    <input type="number" name="a" placeholder="0"><br>
    <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];
$c= "2021";
$b = $c - $a;
echo "Una miaka $b";

 

4. CODE PLAGROUND

Kwa kutumia program hii utaweza kuandika code za html, css na javascript kwenye program hii na kupata matokeo yake yaani preview. Program hii itakusaidia katika kufanya preview ya code zako kujuwa kama umepatia ama laa. Chukulia mfano unaandika <h1>hi</h1> program hii itaonyehsha hi yaani kile ambacho kitapatikana baada ya hizo code za html

 

Kwa kutumia html form <textarea> mtu ataweza kuandika code zake kwenye uwanja huo. Kisha akibofya submit anapata matokeo. Tafadhali kama hujaelewa kwenye fomu za html ana text area rejea course ya kwanza na pili za html.

CODE ZA PROGRAM

<html>
<h1>Code playground</h1>
<form method="post" action="">
<textarea name="a" placeholder="weka code za html hapa"
          style="width: 350px;height: 200px;">
</textarea>    <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];

echo  $a;

 

5. PROGRAM YA KUHESABU MANENO

Fikiria kwa mfano umetoa interview kwa watu 100, na umewataka wajieleze kwa maneno yasiyopunguwa 300. na wote wameandika, hivi utaweza kweli kuhesabu watu wote kuhakikisha kuwa wameandika maneno mangapi?. hapa utahitaji program itakayokuwezesha kuhesabu maneno walioandika.

 

Kwa kutumia program hii utaingiza sentensi ama paragraph au ahabari kisha ukibofya submit unaletewa idadi ya maneno yaliyokuwemo. Hapa nimetumia functino str_word_count() ni php function ambayo tumejifunza katika somo la 5. tafadhali kama utapata ugumu rejea somo la tano.

CODE ZA PROGRAM

<html>
<h1>HESABU IDADI YA MANENO</h1>
<form method="post" action="">
<textarea name="a" placeholder="sentensi ama paragraph hapa"
          style="width: 350px;height: 200px;">
</textarea>    <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];
echo "Idadi ya maneno ni:-";
echo str_word_count("$a");
?>

 

MWISHO WA COURSE

Mpaka kufikia hapa course ya php level 1 ndio nimeifunga. Tafadhalituachie maoni yako ili kuweza kuboresha masomoyetu zaidi na utoaji wa masomo haya. Usiwache kuwa nami kwenye level 2 ya php ambapo tutajifunza zaidi katika yale ambayo tumeyawacha na tutakwenda kuyaona.

 

Kumbuka course zetu ni bure na hatuhitaji malipo yeyote kutoka kwako. Hata hivyo kama utahitaji kufundishwa wewe binafsi nje ya haya mafunzo ya bure bei zetu ni 25,000 kwa kila course. Malipo yatatkiwa kutoka baada ya kusoma vipindi 2. yaani utakuwa na free kwa vipindi 2 kuangalia kama utaridhia na somo na ufundishwaji.

 

 

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass

Web: www.bongoclass.com

Email:mafunzo@bongoclass.com

Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1

 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)
Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi Soma Zaidi...

image Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza. Soma Zaidi...

image PHP level 11 somo la kumi na moja (11)
Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form. Soma Zaidi...

image Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)
hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la tano (5)
Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la kumi na mbili (12) final
Mafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la nane (8)
Hapa utajifunza utofauti kati ya php constant na variable. Na hili ni somo la nane katika mfululizo wa masomo haya ya php level 1. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array. Soma Zaidi...

image Php level 1 somo la saba (7)
Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la kumi (10)
Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement. Soma Zaidi...