Vitu vinavyochochea kuwepo kwa Ugonjwa wa ukimwi.

Posti hii inahusu zaidi vitu ambavyo vinasababisha kuongezeka kwa Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na baada ya watu kujua Ugonjwa huu na matokeo ila bado ugonjwa unazidi kuongezeka.

Mambo yanayosababisha kuongezeka kwa Ugonjwa wa Ukimwi.

1. Kwanza kabisa kitu kikubwa ni watu kutokuwa wazi kuhusu maisha yao.

Kwa sababu watu wengi wanakuwa ni waathirika na wana wapenzi wengi wanaendelea kujamiiana na watu wengine ambao hawana Ugonjwa hali ambayo inafanya kuendelea kuwepo kwa Ugonjwa huu na kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa hiyo uaminifu na uwazi ni lazima.

 

2.Watu wengine kutojali afya zao 

Hali hii inatokea pale ambapo mtu anakuwa anasafiri akifika kituoni yuko radhi kulala na kahaba anayeuza mwili wake bila kutumia kinga ili mradi atulize hamu yake, kwa hiyo hali ya namna hiyo usababisha kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi kila siku na kuwepo kwa Maambukizi mapya.

 

3. Mila na desturi za jamii.

Kuna baadhi ya mila na desturi ambazo Usababisha kuenea kwa Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi, mila hizo ni pamoja na kuridhishwa mke au mme wa marehemu aliyefariki kwa Ugonjwa wa Ukimwi na pia yule aliyeridhishwa utakuta naye ana wapenzi wengine na wapenzi wana wapenzi wengine hali ambayo Usababisha kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

4.umaskini katika jamii.

Umaskini pia nao unasababisha kuwepo kwa ongezeko la Ugonjwa wa Ukimwi kwa sababu unaweza kukuta familia moja wanatumia wembe mmoja, pini na vitu vyote vya ncha kali vinatumiwa na pia kama kuna mgonjwa ambaye yuko katika hatua ya nne ya Maambukizi wanahudumia kwa kutumia mikono bila kujikinga.

 

5. Pia kwa upande wa umaskini unakuta tajiri analala na watoto wa shule na wengine ambao hawasomi kwa lengo la kuwapatia hela kidogo ya kununua matumizi yao ya kawaida na watoto wanakuwa tayari kufanya hivyo ili wapate mahitaji yao yanayokosa kwenye familia zao



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/12/Tuesday - 03:26:42 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1080


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-