Mabaka yanayowasha chini ya matiti.
Posti hii inahusu zaidi mabaka yanayowasha chini ya matiti, ni ugonjwa ambao uwapata wanawake walio wengi na wengine hawajapata jibu Sababu zake ni zipi na pengine uchukua hatua za kutumia miti shamba wakidai juwa hospitalini nugonjwa huu hautibiwa, ila n
Tatizo la mabaka yanayowasha chini ya matiti.
1. Tatizo hili kwa kawaida linaweza kumpata mwana mke yeyote yule hasa hasa uwapata wanawake walio wanene , wanawake wenye Ugonjwa wa kisukari, wanawake wenye matiti makubwa, wanawake wanaofanya mazoezi sana na pia wale wenye pilika pilika nyingi.
2.Ugonjwa huu utokea pale ambapo kuna misuguano kutoka sehemu mbili za matiti zinazoangaliana , baada ya sehemu hizo kubwa na msuguano kwa sababu ya shughuli mbalimbali au wakati wa mazoezi na hewa kwenye sehemu hiyo uwa kidogo hali ambayo Usababisha kuwepo kwa michubuko.
3.Kwa sababu ya michubuko ambayo huwa kwenye sehemu za matiti Usababisha wadudu kama vile bakteria na virusi kuweza kuingia kwenye michubuko hiyo kwa hiyo mama anaanza kuwasha na kujikuna hali ambayo Usababisha michubuka chini ya matiti.
4. Na kwa wakati mwingine kama kuna unyevunyevu kwenye matiti ukachanganyikana na wadudu hao hali inaweza kwa ngumu zaidi na kusababisha kujikuna sana , tatizo hili huwa kubwa zaidi hasa kwa wanawake wale wanaoshinda kwenye shughuli za kutumia nguvu na hawaogi hali huwa ngumu kwa sababu unaweza kukuta matiti yamechubuka sana.
5. Kwa hiyo baada ya kujua tatizo hili wanawake wote hasa kama ni wanene au wembamba ni vizuri kusafisha kwenye sehemu za matiti kwa maji safi na sabuni ili kuepuka na tatizo hili kwa sababu chanzo hiki ni kutofanya usafi na pia wanawake wenye Ugonjwa wa kisukari wawe makini sana kwa sababu walipatwa na tatizo hili ni vigumu kupona haraka kama wale wasio juwa na kisukari.
6.Pia ikumbukwe kwamba kwa akina Mama wanaopiga mazoezi kila siku au kufanya kazi zenye nguvu kama vile kulima kwa mda mrefu wanapaswa kuiga kila siku walau kwa mara moja na kunywa maji mengi ili kuepuka tatizo hili la kuwashwa kwenye matiti.
7.Pia kama imetokea mtu akapata na Ugonjwa huu anapaswa kutumia dawa kutegemea na kisababishi kama waliosababisha ni bakteria Mgonjwa anapaswa kutumia dawa ambazo ni antibiotics kama vile benzathine penicillin, erythromycin, oral penicillin kwa ajili ya kuondoa Maambukizi.
8.Pia Mgonjwa anaweza kutumia dawa iwapo kisababishi ni fungusi anaweza kutumia dawa zinazotibu fungasi kama vile cream zinazotibu fungasi na pia katika matumizi ya dawa hizi hazipaswi kutumiwa kiholela zinatumiwa kwa ushauri wa wataalamu wa afya kwa sababu mtu unaweza kutumia dawa huku una Ugonjwa mwingine hali ambayo inaweza kusababisha matatizo mengine makubwa.
9. Vile vile kwa wale wenye imani potofu juu ya ugonjwa huu waache kwa sababu watu baada ya kupata tatizo kama hili hawakubali kwenda hospitalini na kuanza kutumia miti shamba ambayo uchukua mda mrefu kutibu tatizo na tatizo linaendelea kuongezeka kila siku hali ikiwa mbaya ndipo wanakumbuka hospitali na unakuta wadudu wanakuwa wameingia mpaka ndani na kusababisha madhara makubwa.
10.Kwa hiyo akina Mama huu ni ugonjwa wa kawaida tu na unatibika ukipata tatizo nenda moja kwa moja hospitali ili uweze kupata matibabu kwa sababu Ugonjwa huu umewapa eatu wengi wametibiwa na wamepona na wanaendelea vizuri na maisha.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 web hosting 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Kazi ya homoni ya testosterone
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya testosterone, hii homoni kwa kiwango kikubwa ukutwa kwa wanaume ndiyo homoni ambayo umfanya mwanaume aonekane jinsi alivyokuwa na sifa zake zote.
Soma Zaidi...Jinsi ya kushusha homoni za kiume.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza homoni za kiume kwa akina dada.
Soma Zaidi...Hatua kwa hatua: Jinsi ya kulea ujauzito katika miezi tisa.
Safari ya ujauzito ni ya kusisimua, yenye mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia. Kulea ujauzito kwa usahihi ni uwekezaji wa afya ya mtoto na mama. Mwongozo huu unatoa hatua kwa hatua jinsi ya kulea ujauzito katika kila trimester ili kuhakikisha mtoto anakuwa salama na mama anabaki na afya njema.
Soma Zaidi...Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji
Soma Zaidi...Mambo yanayodhihirisha afya ya nguvu za kiume
Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali yanayodhoofisha afya za wanaume, kwa wakati mwingine wanaume ukosa kujiamini kwa sababu ya mambo ambayo yanaadhiri afya za wanaume.
Soma Zaidi...