8.UTARATIBU WA LISHE KWA WAJAWAZITO NA WANAONYONYESHA.
Wamama wajawazito na wanaonyonyesha. Wanaonyonyesha na wajawazito wanahitaji kupata vyakula vyenye viinilishe vya kutosha ili kuwezesha ukuaji wa mtoto tumboni , utengenezwaji wa maziwa na kwa ajili ya afya zao wenyewe.
Vyakula vya protini vinahitajika kwa mkiwango kikubwa ili kuwezesha mwili wa mama kujenga misuli vizuri , tishu katika mwili wake na mwili wa mtoto aliye tumboni. Utengenezwaji wa maziwa , usafirishwaji wa damu na ukuaji wa viungo vya mama na mtoto unahitaji protini. Hivyo wamama hawa wapewe protini kwa wingi.
Vyakila vya folic asid na vitamini B vinahitajika kwa ajili ya kuwezesha kupunguza tatizo la kushindwa kujifunguwa kwa njia ya kawaida. Vyakula vya madini ya kashiam(calcium) ni muhimu kwa ukuwji wa mifupa ya mtoto aliye tumboni na kuimarika mwili wa mama pia. Kwani mjamzito asipopewa madini haya mtoto atatumia madini yaliyomo kwa mama na kumfanya mama awe na mifupa dhaifu katika kipindi hiki.
Madini ya chuma ni muhimu katika utengenezwaji wa damu, halikadhalika mtoto anahitaji madini haya ili ayatumie katika wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Madini ya zink ni muhimu katika kuwezesha kujifunguwa.(progression of labour) na ukuaji salama wa mtoto aliyoko tumboni.
Wamama wajawazito wapewe vyakula vyenye kambakamba (dietary fiber}. Hivi vitamuwezesha kutopata tatizo la kukosa choo.