7.UTARATIBU WA LISHE KWA WAZEE
Wazee Wazee hawahitaji kuPewa vyakula vya kutia nguvu kwa wingi. Wapewe vyakula vyenye kambakamba ili kuwapunguzia tatizo la kukosa choo na kuwezesha mmeng'enyo wa chakula.

Wazee wapewe vyakula vyenye madini ya chuma, zink na kashiam(calcium) ili kupunguza uwezo wa kupata tatizo la anaemia. Pia madini ya zink ni muhimu katika kuufanya mwili uweze kujenga kinga ya mwili (immune system) na kusaidia kupona kwa urahisi na haraka kwa majeraha.

Ili kupunguza tatizo la kuchoka kwa mifupa (mifupa kuwa dhaifu) kwa wazee wanatakiwa wapewe vyakula vyenye vitamini D na madini ya kashiam(calcium) kwa wingi.

Pia wazee wapewe vyakula ambavyo ni rahisi kutafuna na kumeza. Hii ni kwa sababu wazee wao huwa meno na mifupa yao ni midhaifu pia wana upungufu wa uzalishaji wa mate midomoni mwao kwa mfano baada ya kuwapa nyama wapewe maini.