Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
MAANA YA AFYA
Afya ni hali ya kuwa mzima kimwili na kiakili. Kuna mahusiano makubwa kati ya kuwa mzima kimwili na akili. Mtu anaweza kuwa mwili upo mzima kabisa lakini akaambiwa hana afya salama kwa maana anaweza kuwa akili yake haipo vizuri. Kuathirika kiakili pia ni ugonjwa na ndio maana kuna wagonjwa wa sikolojia.
Hivyo mtu mwenye afyqa ni yule a,baye ni mzima wa mwili na akili. Na tunaposema akili haimaanishwi mgonjwa wa akili ni yule mkichaa hapa na bali hata ambaye saikolojia yake haipo vizuri nae ni mgonjwa.
Ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo ambayo hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa mwili haudhuriki kimwili na kiakili. Mifumo hii ipo kazini muda wowotw kupambana na mamilioni ya wadudu hatari waliopo kwenye mazingira yetu. Kwa mfano kwenye hewa kuna mabilioni ya wadudu kama bakteria ambao huambukiza maradhi.
Mwili unaweza kuthibiti maradhi kupitia njia zake nyingi kwa mfano;- katika mfumo wa damu kuna seli hai nyeupe za damu hizi zinapambana na vijidudu vya maradhi. Halikadhalika mna katika damu antibodies hizi zinafanya kazi hii pia. Kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuna asidi ambazo zinakazi ya kuuwa bakteria na vijidudu vingine vya maradhi. Kwenye mfumo wa upumuaji kuna uttelezi na vijinywele ambavyo hukamata vijidudu pamoja na mavumbi na kutolewa nje.
Hivyo mwili una mfumo madhubuti kabisa wa kuweza kupambana na maradhi. Na ikitokea umepambana na kushindwa hapo hutokea mtu akaumwa. Pia ijulikane kuwa kinga za mwili zinaweza kutengenezwa na mwili wenyewe au kuzipata kwa kutumia chanjo. Mwili huanza kutengeneza kinga hizi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto na hivyo hivyo mwili huendelea kuzitengeneza kinga hizi wakati wa kukua na kuendelea kwa maisha baada ya kuzaliwa.
Pia wakati mwingine mapambano yanapokuwa makali ndani ya mwili huweza kutokea maumivu katika sehemu za mwili. Kwamfano mfumo wa lymph unapopambana vikali huweza kusababisha maumivu ya mtoki.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Hiki ni kitabu kilichosheheni masomo zaidi kuhusu Afya yako, vyakula pamoja na maradhi sugu.
Soma Zaidi...