Namna ambazo Allah hujibu dua ya mwenye kuomba.

Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu.

NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA. Itambulike kuwa dua ambayo imefata vigezo na masharti ya dua itajibiwa tu. Ila pia itambulike kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni kupewa alichoomba, kufutiwa madhambi au kulipwa siku ya qiama kwa kuingizwa peponi.

 

Hivyo itambuluke kuwa mtu anaweza kuomba dua kisha asijibiwe huenda Allah anataka kumpa kheri zaidi au huenda ameshamjibu kwa kumfutia madhambi yake. Allah ndiye anaejua lile ambalo ni bora kwa wajawake katika wakati wowote ule.

Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ ‏"‏ “ “mtu yeyote anaeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa haphapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake kwa kiasi kile alichoomba, maadam hajaomba (jambo la) madhambi au kukata udugu aua hajafanya haraka ya kutaka kujibiwa hata akawa anasema ‘nimemuomba Mola wangu na hakunijibu’”. (amepokea tirmidh).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 2069

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana: