SWALA YA MTUME Kumswalia Mtume (s.
SWALA YA MTUME
Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:
“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amani”. (33:56)
Pia katika maana ya hadithi nyingine Mtume (s.a.w) amesema kuwa bahili ni mtu ambaye atatajwa Mtume (s.a.w) kisha asimswalie.
Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).
“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).
Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;
“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”
Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.
Umeionaje Makala hii.. ?
MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua.
Soma Zaidi...