Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye ngozi wakati wa ujauzito, ni mabadiliko yanayotokea kwenye ngozi ya Mama wakati wa ujauzito.
Mabadiliko ya ngozi wakati wa ujauzito.
1. Kuanzia wiki ya tatu ya ujauzito asilimia tisini ya wanawake wengi miili yao uwa na weusi fulani hii ni kwa sababu ya homone ambayo kwa kitaalamu huitwa melanocyte na kwa sababu ya kazi ya progesterone na oestrogen homoni hizi homoni ufanya sehemu za mwili kuwa nyeusi.
2.Msitari mweusi ambao unaanzia kwenye ambao kwa kitaamu huitwa linea nigra uonekana kwenye sehemu za tumbo huu stari huwa mweusi na uwepo mpaka pale Mama anapojifungua ndipo huu msitari upotea taratibu na baadae kutoweka.
3. Wanawake wengine huwa na Alama usoni ambayo kwa kitaalamu huitwa melasma or mask of plegnant, hizi Alama uwapata wanawake wajawazito ingawa sio wote, Kuna wanawake wengine wanaweza kuwa na Alama ambazo baadae watoto wanaweza kuzaliwa nazo kama Alama za wazazi wao.
4. Kwa sababu ya kuongezeka kwa tumbo la Mama akina mama wengine ngozi zao ujivuta kabisa na kusababisha Alama fulani kwa baadhi ya wanawake ambazo kwa kitaalamu huitwa striae gravidarum kwa sababu ya kuongezeka kwa Tumbo la Mama, hizi Alama upotea taratibu pindi Mama akimaliza kujifungua.
5. Kuongezeka kwa kiasi kikubwa Cha damu kwenye mwili hali hii uoneka kwa baadhi ya wanawake ambapo mishipa uonekana mpaka juu kuliko kawaida, kwa Sababu ya kuongezeka kwa damu kwenye ngozi na damu ukimbia sana kuliko kawaida kwa hiyo joto la wanawake uwa juu sio kwa ajili ya ugonjwa Bali ni joto linalosababishwa na wingi wa damu na mishipa kwenye ngozi ya Mama mjamzito.
6. Wanawake wakiona dalili zote hizi kwenye ngozi wasishangae kwa sababu ni hali ya kawaida inayotokea kwenye mwili pindi Mama anapobeba mimba na zile jamii ambazo zina Mila na desturi ambazo hazieleweki kwa dalili ambazo ujioshesha kwa akina Mama wajue kuwa ni kawaida na utokea wasitumie vitu vingine ambavyo umfikisha Mama kwenye hali ngumu na mbaya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza homoni za kiume kwa akina dada.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga
Soma Zaidi...Ujauzito husababisha mabadiliko mengi mwilini, ikiwepo ongezeko la Majimaji ukeni ifikapo tarehe za kukaribia kujifunguwa. Majimaji haya ni muhimu kwa afya ya mtoto aliye tumboni.
Soma Zaidi...Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Yai lililopikwa ni chanzo kizuri cha protini, vitamini, na madini muhimu kwa mama mjamzito. Husaidia katika ukuaji wa mtoto tumboni, afya ya mama, na kuimarisha kinga ya mwili.
Soma Zaidi...ukiwa na ujauzito unaweza kuona mabadiliko mengi katika mwili wako yakiwemo kutokwa na majimaji. je majimaji haya yana dalili gani kwenye ujauzito?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo
Soma Zaidi...