Afya inaweza kuathiriwa na vitu vingi sana. Hapa tutaendelea kuona mabo zaidi yanayoathiri afya yako.
4.TABIA
Tabia za watu pia zinaeza kuwa ni sababu ya kupata maradhi na kuathiri afya. Watu wamekuwa wakikulia katika koo, familia na kabila mbalibali ambapo wanajifunza tabia tofautitofauti. Tabia hizi kama hazitakuwa katika hali inayotakiwa zinaweaa kusababisga kupata maradhi
Nitoe mfano mzuri kuhusu maradhi ya fangasi sehemu za siri. Fangasi hawa wanafurahia sana mazigira yenye majimaji. Mara nyingi usafi wa nguo za ndani na mwili kwa ujumla hususan sehemu zile umaweza kuwa sababu ya kuendelea kuwalea wadudu hawa. Tabia ya kuvaa nguo mbichi hususani zile za ndni inaweza kuendelea kuwalea fangasi hawa.
Tabia ya kula mara kwa mara inaweza kusababisha kupata kitambi. Mtu akiwa anakula mara kwa mara bila ya kufanya mazoezi anaweza kupata tatizo la kuzidi kwa uzito. Tatizo hili linaweza kuathiri mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulin kwa kiwango kinachotakiwa na hatimaye kupata kisukari.
Tabia ya kuchelewa kualal yaani kukosa muda mzuri wa kulala inaweza kuwa sababu ya kupata matatizo ya kiafya. Mwili unahitaji muda wa kutosha wa kulala ili uweze kurekebisha mwili ndani ya muda huo. Mwili unahitaji kupumzika pia.
Tabia ya kukaana misongo ya mawazo na kupenda kukasirika na kukaa na vinyongo. Hii ni hatari sana ka afya ya mtu kisaikolojia na kimwili pia. Misongo ya mawazo inaweza kuwa sababu nzuri ya kupata maradhi kama vidonda ya tumbo. Maumivu ya kichwa na tumbo pia huweza kuletwa na misongo ya mawazo
5.VIZAZI, FAMILIA NA KURIDHI (GENETICS)
Afya ya mtu inaweza kuathiriwa na kurithi kutoka kwa wazazi. Hapa mtu hana chaguo maana kurithi huku kumetokea toka tumboni kwa mama. Mtu anaweza kurithi maradhi kama pumu, moyo, kisukari, siko seli na mengineyo.
Kwa ufupi hivi vipengele vinavyoathiri afya tutaviona kwa undani zaidi kwenye kurasa zijazo. Hapo tumeona tuu juu juu namna ya mabo yalivo. Sasa hebu tuone vitu tutaweza kuboresha afya zetu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukuletea mfumo wa damu mwilini na safari zake za Kila siku
Soma Zaidi...Kama unapatwa na maumivu ya tumbo na ilhali mkojo ni mchafu, ama una harufu sana, basi post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...