Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

KISIWA CHA UOKOZI

Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli. Na kwa kuwa miguu yangu haikuwa na nguvu nilibuluzika tu. Nililala bila ya kijitambua niliamshwa na maji yaliyokuwa yakinipiga miguuni kumbe maji yalikuwa yanajaa. Haukupita muda ghafla nikaona kuna kijahazi kinaingia kikiwa kina mifugo kadhaa. Walipofika pale kisiwani wakawafungulia mifugo yao na kuanza kuwaosha na kuwapaka dawa. Mmoja wao akaenda mbali kidogo akaja na majani mengi sana na kuanza kuchagua baadhi ya ng’ombe na kuanza kuwapa majani yale.

 

Niliwafuata na kuwaomba msaada wa chakula. Wakanipa maziwa na mkate wa nyama. Nilipomaliza kula wakaniuliza habari yangu na eneo lile na nikawaeleza kila kitu. Basi wakaniambia kama ungekuja kesho usingetukuta na pengine ungefia hapa maana hakuna majahazi yanayokuja hapa ila ni sisi tu na huchukuwa miezi 3 ndo tunakuja tena. Na kisiwa hiki hakina chakula, hivyo pengine ungeishia kufariki hapa. Basi wakanipatia na nguo na nikawauliza pia sababa ya wao kuja hapa na ni kinanani wao.

 

Mkubwa wao akanieleza kuwa wao ni watumishi wa mfalme aliyepo karibu na eneo hili. Mfalme huyo amekiteua kisiwa hiki kama eneo la kutibia mifugo yake na amepanda majani maalumu kama dawa ya mifugo yake. Hivyo eneo hili hawaruhusiwi watu wengine hapa. Basi walipomaliza shuhuli zao walifunganya mizigo yao na kuchukuwa majani mengi na nikaondoka pamoja nao.

 

Tulipofika kwenye utawala wao wakanipeleka kwa mfalme wao na nikamueleza mimi ni nani na nini kazi yangu na kumueleza kuwa natokea baghdada nchini kwa sultan Harun Rashid. Basi mfalme yule nikamueleza mengi kadir alivyouliza na mimi sikuwacha kuu;liza mambo kadhaa. Kwa haraka zaidi mfalme yule alionekana kunipenda sanan na kunikubali. Basi alinifanya katika watu wa karibu yake na ni kama mshauri pia. Niliishi pale nikawa nafanya biashara chini ya mfalme yaani nilikuwa naendeleza bishara za mtoto wake wa kike.

 

Siku moja niligundua kuwa kuna kisiwa jirani ambapo kunasikika sauti za furaha kila siku. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ni kisiwa jirani huwa wannafanya sherehe kila wanaporudi kutoka kutafuta lulu. Hicho ni kisiwa pekee kinachofahamika kwa kuwa ni wafanyabiashara wa lulu. Basi kwa kuwa sikuijua lulu ilibidi niumuombe ruhusa mfalme ili na mimi nikashuhudie sherehe zao na nipate kuijua lulu. Mfalme alikubali na akanipa msafara wa wafanyakazi wake waende pamoja nami.

 

Tulipofika kule nilifurahi kuiona lulu kwa mara ya kwanza na nikafurahia pia sherehe zao. Basi katika hali kama zile nilishangaa kuona kuwa watu wanashusha mizigo kutoka bandarini lakini katika ile mizigo kuna ambayo imeandikwa Sinbad, nilipoangalia kwa uzuri nikagundua kuwa nahodha wa lile jahazi alikuwa ni yule nahodha wetu. Hivyo kumbe zile mali zilikuwa ni zakwangu na lile jahazi lilikuwa ni lile letu. Nikamuita kijana mmoja na nikamuuliza habari zao na akanieleza kuwa walibahatika kuliokoa jahazi lao na watu wote walipona isipokuwa Sinbad ndo hakuonekana. Kijana huyu alizungumza bila ya kunijuwa kama ndo mimi

 

Basi nikamfuata nahonda na kumueleza kuwa mimi ndo Sinbad na zile mali ni za kwangu. Basi nahonda alliponiona akanikumbuka na kutoa machozi kwa furaha maana walifahamu kuwa nimekufa. Nahodha akanikabidhi mali zangu na nikaziuza, nikapata habari kuwa jahazi letu litarudi Baghdad wiki ijayo. Nilichukua bidhaa zangu na kuuza baadhi na kurudi kwa mfalme na baadhi ya bidhaa. Nikamuelezea kilichotokea na alifurahi sana kwa kupata bidhaa zangu. Na hivi ndo Mwenyezi Mungu anavyowafanyia watu wenye subira.

 

Nikampatia mfalme bidhaa zilizobaki kama zawadi na nikamuomba ruhusa ya mimi kurudi nyumbani kwetu wiki ijayo. Kwa majonzi na kinyongo mfalme aliniruhusu na hata binti yake alikuwa na majonzi sana lakini haina budi “milima haikutani binadamu hukutana” ni maneno nilojisemea moyoni. Basi wiki ilipoisha mfalme alinipatia mali nyingi sana kama zawadi. Nilipata pia lulu kutoka kwenye kisiwa kile. Kwa hakika katika safari hii nilipata taabu na faida kubwasana.

 

Tulipofuka Baghdadi niliwaelezea ndugu zangu habari ya yalonikuta, kwakweli waliniambia niwachanena habari za biashara hii. Hata mimi nikajiapiza kwa yalonikuta kwa hakika sitarudia tena bishara hii. Basi nikatoa sadaka kutoka katika faida yangu na nikatoa na zaka muda ulipo fika. Nilitumia faida ile kujiendeleza kibiashara hata miezi mingi ikapiata. Nilisahau kabisa yalonikuta kwenye safari ile. Baada ya muda nahodha wetu wa mwanzo nilikutana nae, na katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa wanatarajia kuanza safari wiki ijayo.

 

Kwa hakika nilivutiwa tena na biashara ile. Na kwa kuwa nilisahau machungu yalonikuta katika safari ya kwanza nikaazimia kuanza safari ya pili wiki ijayo. Mpaka kufikia hapa Sinbad kwa baharini akamaliza kusimulia hadithiya safari yake ya kwanza. Na kwa kuwa muda ulukuwa umekwenda hakuweza kuanza hadithi ya safari yake ya pili. Basi akampatia Sinbad mbeba mizigo zawadi nyingi na pesa kadhaa ya kutumia kama fidia ya kuvunja kazi zake. Na akamuahidi kesho awahi kuja maana safari ya pili ina mambo mengi na makubwa zaidi kuliko ya kwanza.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 822


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

SAFARI YA MUUJIZA ( SEHEMU YA PILI)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ya safari yenye muujiza ,ni pale mtoto ya Mungu mengi anafika kwenye kituo Cha ntonga na kuona yake mazingira na kufahamu njia ya kwenda kule. Soma Zaidi...

Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya mfalme na waziri wake
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Usichofahamu kuhusu mazoezi
Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo hufahamu kuhusu mazoezi,ni mambo ambayo utokea au no matokeo mazuri kwa watu wanaofanya sana mazoezi. Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na kijakazi wa sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Khalid mwenye kuneemeshwa na Jalid
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...