picha

Safari ya kwanza ya sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

SAFARI YA KWANZA YA SINBAD

Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid. Baba yangu alifariki miaka 21 iliyopita nilipokuwa kijana kama wewe. Wakati huo nilikuwa na marafiki wengi sana. Na nilianza kutumia mali aloniachia baba na hatimaye akakaribia kuisha na marafiki wakanikimbia. Na hapo ndipo nilipoamua kuanza biashara za majini, yaani kuuza bidhaa sehemu mbalimbali za visiwa.

 

Nilijiandaa vizuri kwa ajili ya safari yangu ya kwanza. Na maandaliizi yalipokuwa tayari tulianza safari ya kubiashara. Safari ilikuwa salama kabisa kwa muda wa masiku. Tulipita visiwa kadhaa tukiuza na kununua. Kwa upande wangu biashara haikuwa mbaya ijapokuwa ugeni ulinisumbuwa sana. Kwa ujumla nilifurahia safari ile. Baada ya kutembea visiwa kadhaa tuliamua kumalizia katika viziwa vingine ili tuweze kurudi nyumbani. Ilitikea sikumoja ghafla upepo ulianza kubadilika na jahazi likashindika na kudhibitiwa na manahodha.

 

Upepo ulizidi mpaka nahodha akaamua kukiachia chombo kiende kokote, hali iliendelea kuwa mbaya mpaka bidhaa zikaanza kutumbukizwa majini ilikuokoa ualama wa maisha. Haliiliendelea kuwa mbaya hata chombo kikaanza kunywa maji. Watu wakaanza kuania rohozao, na kuanza kushika mbao zilizovunjika kutoka kwenye jahazi. Mimi nilipata mbao moja na ilinipeleka mbali zaidi ambapo sikuweza kuona hali za wenzangu kilicho endelea.

 

Kwa upande wangu mawimbi ya maji yalinipeleka mbali sana, nikiwa nimeshikilia tawi lile hata sikusubutu kuliachilia. Nilipofika hali ambapo sijielewi kwa kuchoka ghafla nikaona kunaweupe mbele yangu, kuangalia vizuri kilikuwa ni kijisiwa kidogo. Basi nikajitahidi kujizuia huku nikawa naiba maji ili yanipeleke kule. Kwa bahati njema kaupepo kakanipeleka kwenye kisiwa kile. Kwa msaada wa mizizi ya miti niliweza kutoka kwenye maji yale.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views 2201

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 ai web app     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 web hosting     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Safari ya sita ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Kutokana nyani mpaka kuwa chongo

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya binti wa pili mwimba mashairi mwenye makovu

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...