Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.

Mimi ni mtoto wa mfalme wa nchi hii ambayo umemuona amegeuzwa jiwe kama watu wengine. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikilelewa na bibi mmoja laiyekuwa ni muiislamu. Watu wa mji huu walikuwa wanaabudu masanamu hivyo bib i yule alifanya siri imani yake. Na kwa usiri huo akanifundisha imani ya uislamu juu ya mungu mmoja na akanifundisha kusoma Qurani. Katika muda wote niloishi nae yapata miaka 10 alikuwa akinisisitiza kufanya siri imani ile na mambo yakawa hivyo mpaka bibi yule alipofariki.

 

Mwaka juzi alikuja mtu mmoja hapa nchini kwetu, mtu huyu ulikuwa ikilingania watu kuhusu kumuabudu mola mmoja tofauti na watu walivyozoea. Mfalme aliongea maneno ya ajabu na ya kipuuzi kuhusu sauti ile. Mtu yule aliondoka na akarudi tena mwaka jana na maneno yalikuwa ni yalelyale. Na mfalme yaani baba yangu alirudia maneno yaleyale. Na mara ya tatu mwaka huu alirudi tena Mtu yule na mambo yakawa vile vile.

 

Wiki mbili baada ya kuondoka kwa Mtu yule ikatokea sauti ikionya na kulingania juu ya imani ya munngu mmoja. Hali ikawa kama mwanzo Mfalme wetu akatoa kejeli na maneno machafu sana. Kwa hakika niliumia na nikataka kwenda kumtia adabu baba yangu mwenyewe lakini nilishindwa kufanya hivyo. Machozi yalinitoka na nisijuwe jambo la kufanya na hakina wa kunishauri. Basi haikupita muda mrefu ile sauti ikatoweka na hapo anga ikafunga kuwa nyeusi kutokana na wingu lisilojuliukana kama la mvua au upepo mkali.

 

Wingu lile liliendelea kusogea chini hata likakaribia kufunika nyumba. Ulikuwa ni wakati wa muda wa swala ya adhuhuri na watu wamechanganyika katika utaftaji. Wengine wapo masokoni na wengine mashambani na hali kadhalika. Wingu lile likaambatana na upepo mlaini ambao haukuweza kuharibu hata kipande cha nguo kilichokuwa kinaning’inia. Upepo ule uliingia masikion, puani na kila sehemu yenye tundu na kutokea upande mwingine.

 

Haukupita muda wat wote wakawa katika hali uloiona kuwa mawe. Na kia mtu vile alivyo ndivyo alivyobaki. Hata walokuwa wamelalaq wamebakia mawe kwenye vitanda. Nilitoka kuchunguza zaidi sikuona hata mnyama ambaye aligeuzwa jiwe. Kwa hakika msiba huu uliwapata wanadamu tuu. Basi nikawa sina pa kwenda hiyo nikabakia kisiwani hapa peke yangu kama unavyonioa. Na hii ndiyo historia ya kisiwa hiki kilichogeuzwa mawe.

 

Wakati kijana anamaliza kusimulia hadithi ile Zubeida akawa analia na machozi yanamtiririka kama chemchem iliyoanzia mlimani. Basi kijana kwa huruma akawa anamfuta machozzi Zubeida. Baada ya muda Zubeida akauliza “sasa wanyama walikwenda wapi?” kijana akamjibu baada ya kutokea yaliyokwisha tokea ilikuja tena ile sauti na kuniambia kuhusu hatima ya wanyama. “ama kuhusu wanyama amri yao ipo kwako, eidha utawatumia kama chakula chako mpaka Allah atakapoleta nusra , ama awahamishe awapeleke anakotaka ama wageuzwe kuwa vitu vya thamani na iwe kama zawadi ya Zubeida mwenye kupotea njia mwana wa tairi na msalitiwa na ndugu zake.

 

Basi nikachaguwa jambo la tatu, na pindi ulivyokuja nilifahamu hakika ni wewe Zubeidah. Zubeida akamuuliza “ni kitu gani kilichokufahamisha” akaendelea ile sauti niliiulisa sasa ni kwa namna gani nitamfahamu Zubeidah ikajibu siku moja kabla ya kuja kwa Zubeiday bahari itakuwa chafu sana na upepo maini utaingia kisiwani hapa na kusafisha nyia ya Zubeida mwana wa tajiri, msalitiwa. Hivyo Zubeida atakuwa hana jinsi ila atakufikia tu popote utakapokuwepo muda huo. Basi nilipoziona ishara hizo nilifahamu ujio wako hivyo ili kukurahisishia kunipata nikawa nasoma Qurani kwa sauti ya juu ndivyo ukanisikia.

 

Ama kuhusu kusalitiwa kwa Zubeida na ndugu zake nilishindwa kujuwa mengi zaidi maana sauti ile ikanambia hainipasi kujuwa siri za mambo yajayo. Halikadhalika ninachofahamu zaidi kuhusu huo usaliti ni kuwa maisha yangu ama yako yatakuwa hatarini. Basi Zubeida na yule kijana wakatoka pale na Zubeidah akashauri waoane na wakakubaliana kufunga ndoa punde watakapofika nyumbani.

 

Basi kijana akampeleka Zubeidah kwenye zawadi yake na akakuta mali nyingi sana na tayari imeshafungwa vizuri kwenye mkokoteni. Basi wakaburuza mkokoteni wao mpaka kwenye chombo chao na kuuingiza ndani. Wakawa wanapunga upepo ufukweni na kubadilishana mawazo na kuchat. Wakiwa katika hali hiyo ghafla akatokea nge anakimbizwa na kunguru Zubeidah akachukuwa kijiwe na kumpiga kunguru na ukawa ndio mwisho wa maisha ya kunguru yule na nge akatokomea kwenye mawe. Na wawili hawa wakaendelea kuzungumza. Wakati yote haya yanafanyika dada zake na Zubeidah walikuwa wakiona wivu na kijicho kwa mafanikio ya ndugu yao.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1029


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

USALITI (sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelzo wa hadithi ya Usaliti kati ya Rhoda na Moses ambapo Moses anampenda sana Rhoda na wakati wa kuoa umefika ila akagikilia kwamba akimuoa Rhoda inawezekana wasipate watoto kwa sababu ya mimba ambazo Rhoda alikuwa anatoa mara kwa mara. Soma Zaidi...

Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 4)
Posti hii inaendelea kuelezea hasara za kuwepo kwa wivu na kutokuwa wazi katika, jamii inafikia wakati baba anapifahamu ukweli anawaita wazazi wawili na kuwaombeza kwa kuwa kimya baada ya kuona matatizo yaliyokuwa yanampata mtoto Lisa. Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi. Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya mke na kasuku
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mtihani unafika ila Jackie hakujiandaa alishutuliwa na marafiki zake baada ya kuona mwenendo wake haueleweki. Soma Zaidi...

Dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...