Safari ya pili ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

SAFARI YA PILI YA SINBAD

Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Walipokusanyika watu wote vikaagizwa vinywaji na vileja na kuanza kula huku wakisikiliza hadithi. Sinbad wa baharini akaanza kusema “basi tambueni kuwa sfari hii ya pili nilikutwa na makubwa zaidi kuliko hii ya kwanza. Ha ilikuwa hivi:-

 

Basi tulipozungumza na nahodha kuwa wiki ijayo wataanza safari nilirudi nyumbani na kujiandaa kwa safari. Ndugu zangu walijaribu kunizuia lakini sikuwasikia “sikio la kufa halisikii dawa” wengine wakanambia najipeleka nikafe ila sikuwasikiliza. Maandalizi yalikamilika kwa siku mbili na nikawa nasubiria safari tu. Wiki ilipofika tukaanza safari kwa amani lakini siku ya tatu kabla ya kuingia kisiwa cha kwanza kufanya biashara hali ya hewe ikabadiliki ghafla.

 

Nikiwa na woga sana juu ya roho yangu nikabaki namuomba msamaha mwenyezi Mungu. Jahazi lilikwenda ovyo ovyo kwa muda wa masaa sita. Manahodha walifanya wawezapo hata wakaamua sasa kuachia hatima kwa Mwenyezi Mungu. Abiria tulianza kutapika na mimi nikiwa mmoja wapo. Kwamuda kadhaa nilipotelewa na kumbukumbu na sikufahamu zaidi. Nilikuja kupata fahamu chombo kilianza kutulia mbele yetu kukiwa na weupe kwa mbali. .

 

Nilikaa vizuri nipate lujua kinachoendelea. Manahodha walituambia kuwa kwa sasa tunaingia kisiwa cha roc. Kisiwa hiki hakuna wakazi na wanyama pia hakuna au ni wachache. Kuna hadithi ya zamani sana walokuwa wakisimulia mababu kuwa kuna roc aliyekuwa akila mali za watu kama mifugo na kujeruhi wakazi. Hivyo watu wamehama kisiwa hiki. Ni miaka mingi sasa na ni mababu tu wanasimulia hadithi hii. Huenda ni ngano tuu au ni kweli. Hivyo tutaingia hapa kwa ajili ya kupumzika kidogo na kuangalia kama tutapata maji maana safari ni ndefu.

Basi tukaingia kisiwani pale na kuanza kuranda randa. Kwakuwa nilitapika sana sikuwa na nguvu za kutosha hivyo nikaelekea kwenye kivuli kikubwa na kujilaza. Nililala sana na nilipokuja kuamka sikuona watu wala jahazi. Kumbe nilisha kimbiwa, niliogopa sana na nisijue nitatokaje pale kisiwani ambapo hakuna watu wala chakula. Nilianza kujuta kwa kukubali kuja. Nilijua sasa hapa kisiwani nitakufa pekeangu kwa kukosa chakula.

 

Nilianza kukizunguka kisiwa chote kujua nini nitafanya. Jua nalo lilikuwa likizama. Katika kuzunguka nikaona kuna kitu cheupe kwa mbali. Nikaanza kukifata taratibu na nikakuta kama limpira kubwa sana na laiiini. Kuangalia vizuri sikufahamu nini kitu kile. Ghafla nikaona anga inafunikwa na kuna kivuli kikubwa kinaingia nilikimbia kwenda kujificha. Kumbe alikuwa ni ndege roc mkubwa sana yaani mguu wake mmoja ni kama shina la mti. Kumbe lile dude kubwa jeupe ni yai lake.

 

Basi kiza kilipoingia nilikwenda karibu na ndege yule nikavua kanzu yangu na kufifunga vizuri kwenye miguu ya yule ndege. Niliamini kuwa akiruka atanibeba na kunitoa kwenye kisiwa kile. Basi nilifanya hivyo na kuendelea na imani yangu hiyo. Mambo yakawa kama nilivyotaka asubhi ndege yule aliruka na kunibeba, kwa kuwa sikuwa mzito sana hakujua kama amebeba kitu lamda alijua ni guo tu.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1398

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Hadithi ya tabibu wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA

Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA

Soma Zaidi...
HADITHI YA BINT WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU.

Soma Zaidi...
HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE.

Soma Zaidi...
Binti wa ndotoni

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Safari ya kwanza ya sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Hadithi ya jini

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Kuingia kwa wageni

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Usuluhishaji wa walio dhurumiwa

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...