image

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI.

Mzee wa pili akapewa ruhusa ya kusimulia stori yake na mbwa wawili weusi. “kwanza utambue ewe mkuu wa majini kuwa hawa mbwa unaowaona ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja, stori ilikuwa hivi”

 

Baba yety alikuwa ni tajiri mkubwa katika mji tuliokuwa tukiishi. Alipofariki alituachia mali kubwa na tukaigawa mafungu matatu kulingana na idadi yetu. Tuligawana sawa kwa sawa. Ndugu zangu hawa wakajikita kwenye biashara za nje na ndani ya mji. Wakawa wanasafirisha bdhaa kwenda miji mbali mbali, na hata kwenye visiwa.

 

Mimi niliamua kufungua duka hapa mjini na kwa neema za Allah biashara ikawa nzuri. Mali yangu ilifikia mara tatu ya ile niliopata kutoka kwenye urithi. Sikumoja ndugu zangu walitoka kibiashara, walikaa kwa muda wa miezi isiyopunguwa miwili. Baada ya hapo nikaona kuna watu wawili wamesimama mbele ya duka langu. Sikuwatambuwa watu hawa kutokana na mavazi yao. Walikuwa wamevaa mavazi yaliyochakaa ama yaliyookotwa jaani. Niliataajanu kuona wana nifahamu, baada ya kuzingatia zaidi nikagunduwa ni ndugu zangu.

 

Nikawapa mavazi na chakula kisha wakanihadithia mkasa wao. Walikuwa wamepata ajali na malizao zote zimetokomea majini. Nikachukuwa ile faida yangu na nikaigawa sasa kwa sawa kati yao. Wakaanza biashara tena na hawakukoma baada ya muda wakaamua kusafiri tena kibiashara. Hali ilikuwa mbaya zaidi wakati huu. Walipata ajali tena majini na wakktupiwa nchi kavu wakuiwa hata mavazi hawana.

 

Niwalipfika nyumbani sikuwatambuwa kwa kuwa walikuwa uchi na wakiwa wamechafuka ngozi zao. Wakajitambulisha na niliilia kwa huruma. Machozi yangu nhayakufaha kitu kwa kuwa tayari jambo lilisha tokea. Kama mara ya kwanza nikawapa mtaji na wakaanza upya biashara zaoi. Baada ya muda biashara zao zikakaa vizuri, na wakaamuwa kutoka tena kibiashara. Ila mara hii walitaka niende pamoja nao. Nilipinga zaidi safari hii lakini walinilazimisha na hata maandalizi pia wakanifanyia.

 

Sikuwa na jinsi nikajiandaa na mimi kwa safari. Nikachukuwa mali zangu nikazigawa sehemu mbili na sehemu moja nikachukuwa na nyingine nikaificha. Safari ilianza vizuri na tulifika miji mbalimbali tukifanya biashara. Nilipata faida kubwa na nikanunuwa baadhi ya bidhaa ambazo ningeziuza pindi nitakapo rejea.

 

Muda wa kurudi uliwadia tukawa tunaanda safari ya kurudi. Nilipokuwa matembezini nikitafuta bidhaa na zawadi za kwenda nazo nyumbani, nilipita ufukweni nikakutana na mwanamke aliyevaa mavazi yaliyo chakaa. Nilimsalimia na akarudisha salamu, nikamchukuwa na kumtafutia mavazi yaliyo mazuri. Kwa mavazi yale uzuri wake ulidhihiri mbele yangu. Kwakuwa sikuwa na mke ilibidi nifuate taratibi za kufunga nae ndoa na akakubali. Maandalizi yote yalipoisha nilimchukuwa mke wangu kurudi nae nyumbani.

 

Tukiwa kwenye jahazi zikugunduwa kumbe ndugu zangu walikuwa wananionea wivu. Wakawa wananipangia njama ya kuniuwa. Ulipofika usiku walinichukuwa na kunitumbukiza majini. Baada ya pale sikujuwa kilichoendelea nikajikuta nipo nchi kavu. Mke wangu akanieleza khabari za yote yaliyotokea na akanieleza kuwa yeye si mtu wakawaida. Akaniambia pia hatoweza kuwasamehe ndugu zangu kwa walichonifanyia. Nilimuomba asiwaue ila nipo radhi kwa adhabu yeyote ile.

 

Alinichukuwa mpaka nyumbani kwangu, kisha akalizamisha jahazi waliopanda ndugu zangu. Mali zangu zote akaziokoa. Siku iliyofata nikiwa nyumbani nikaona kuna mbwa wawili weusi wanakuja huku wakionesha majonzi na hali ya kuomba msamaha. Nilistaajabishwa na tukio hili. Haukupita muda mke wangu akatokea na akaniambia hawa ni nduguzangu amewapa adhabu hii. Watakuwa hivyo kwa muda wa miaka 10.

 

Miaka 10 sasa imefika, na kwakuwa alinielekeza sehemu ya kukutana, ndio nimetoka kuelekea hapo sehemu. Nikaona niwachukuwe ndugu zangu kwa kuhofia kuwaacha kwa mtu asie akawadhuru.

 

Hii ndio stori yangu na mbwa hawa ewe mkuu wa majini. “hii ya kwako inamakubwa zaidi” ni maneno ya jini. Baada ya hapo mzee wa tatu akazitupa miguuni kwa jini na kutaka ruhusa aruhusiwe kughadithia stori yake ili iwe ni kafara ya kuachiwa huru mfanya biashara. Lile jini likasema “hapana nimetosheka na hizi mbili, na nimekubali kumuacha huru mfanya biashara” jini lilizungumza maneno haya na kuondoka.

 

Mfanya biashara akawashukuru wazee wale. Basi wakati wazee wale wapokaribu na kuondoka yule mfanya biashara akamuuliza mzee yule wa tatu mwenye mbwa mwekundu kuhusu habari ya mbwa yule. Mzee akamwambia ni stori ndefu ila kwa ufupi huyu ni mke wangu. Akaanza kusimulia hadithi yake kwa ufupi huku akiwa na haraka ya kutaka kuondoka eneo lile           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1323


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

MWANZO WA USALITI
Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Soma Zaidi...

Hadithi za Sinbad
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya mvuvi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

SAFARI YA NNE YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME. Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya wanawake watatu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MFANYABIASHARA NA JINI
Soma Zaidi...