picha

Ndoa ya Sinbad na binti mfalme

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.

Siku hazikuenda kipolepole hatimaye wiki ikafika na harusi ikafanyika. Sherehe kubwa isiyo na kifani ilifanyika na hata wafalme wa jirani walihudhuria. Niliozeshwa binti yule na kukabidhiwa nyumba ndani ya ikulu. Nilipata kukabidhiwa na mali na mambo mengine kadhaa. Sherehe za kimila pia zikafanyika kwa ajili ya kukabidhiwa cheo cha mfalme ajae yaani baada ya kufa mfalme huyu nitakuwa mfalme mpya. Yote haya yalifanyika japo sikuwa na furaha nayo.

 

Ni miezi miwili sasa imefika na mishaanza kuzoea mazingira ya kulinda muda wote na kuzungukwa na watu. Nilitembelea uwanja wa kujifunzia farasi nikakuta watu wanaendesha farasi bila ya kuweka kiti chha farasi. Basi nikatumia taaluma nilonayo na kuwatengezea viti vya farasi. Jambo hili lilifanya nipendwe sana na watu na mawaziri kwa kuleta kitu kipya zaidi. Mapenzi ya mfalme na mimi yalizidi kuongezeka siku hadi siku. Watu walikuwa wakinikubali sana hasa ninapokuwa nawasimulia hadithi za kuhusu baghadad na safari za majini na mikasa iliyowahi kunikuta.

 

Ni miezi mitano sasa toka kumuoa binti mfalme. Binti mfalme alinipa habari za furaha kuwa ana ujauzito. Nilizipeleka habari zile kwa babamkwe na mama mkwe. Kwa hakika siwezi kusimulia namna ambavyo furahayao ilivyokuwa. Habari ziliwafikia mawaziri na watu wengine. Wote walikuwa wakiniupongeza. Binti mfalme alizidi kuniona mimi ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake kwa kumfanya awe mama mtarajiwa wa familia ya mifalme.

 

Hatimaye miezi ya kujifunguwa ya binti mfalme imefikia na sasa amepelekwa kwa wakunga. Nikiwa nipo mlangoni kusubiria habari za furaha nilishitushwa na kilio kikubwa sana kilichotoka ndani. “Innaa lillahi wa innaa ilaihi rajiun” niliposikia maneno haya yakisemwa nikajua mtoto wangu amefariki dunia. Nilianza kulia sana, na muda si mrefu mkunga mmoja akatokea nje na kuniambia kuwa binti mfalme amefariki dunia na mtoto wake amepona. Nililia zaidi na kutamani ardhi inifukie.

 

Furaha za kupata mtoto sikuweza kuzipata kamwe nikikumbuka kuwa nakwenda kuzikwa na me wangu. Mila haikuwacha kufuata mkonowake sasa mwili wa marehemu ukawa unaanza kuandaliwa na nikamuona baba mkwe akija kwa unyonge na kunipa maelekezo na kunipatia nguo mpya na kuniambia hizi zitakuwa ndio sanda yako. Sina la kukusaidia lamba nitakuongezea mkate wa nane. Maana huwa aliye hai anapozikwa na mwenza anapewa kichupa cha maji na mkate mikate 7 hivyo nitakupendelea kukupa mikate nane.

 

Maneno haya yaliendelea kuniumiza hasa pale watu walipokuja kunihani na kuniaga kwa mara ya mwisho. Sasa ndipo nikaanza kujuta kukubali kutembea majini safari hii. Nilitamani hata ningekuwa kama wale wenzangu nilowaaza kule wanachinjwa maana taabu nitakayoiona na kuzikwa nikiwa hai ni kubwa. Basi likaandaliwa jeneza moja kubwa sana na mimi na mke wangu tukaingizwa na kubebwa kuelekea mazikoni. Walikwenda kwa muda wa masaa 2 na nusu kisha wakaanza kupandisha juu kwa mwendo wa nusu saa. Nikawasikia wanazungumza kuwa wamefika tayari.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views 1563

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 ai web app     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Safari ya majibu juu ya maswali mawili

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
MFUGAJI NA MKEWE

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISA CHA MFUGAJI NA MKEWE.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MWEN YEKUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii.

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama.

Soma Zaidi...
MWANZO WA USALITI

Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani.

Soma Zaidi...
Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...