Ndani ya pango la makaburi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad
NDANI YA PANGO LA MAKABURI
Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.hatimaye n ikahisi jeneza limefika chini kutokana na kugonga chini. Nikalifungua jeneza lile na kutowa mikate yangu nane na maji yangu. Nikaangalia huku na huku hakuna pa kutokea. Nikaangalia juu ni mbali sana na tundu ni dogo na hata sauti haifiki. Nilizunguka mchana mzima sikupata pa kutokea. Sikuya kwanza, pili, tatu mpaka siku ya nne sikupata pa kutokea. Nilikata tamaa nikajua sasa huu ndio mwisho wa Sinbad.
Nikaanza kula mikate yangu kwa kuilinda ili isiishe kwa araka. Sasa imefika siku ya sita nikiwa na mikate miwili mkononi. Ilipofika siku ya saba mida ya mchana nikasikia migongano. Nikasogea karibu kwenye lile tundu loo!! ni jeneza linakuja. Nilikuwa nikihisabu siku kwa kuangalia mwanga kwenye tundu lile dogo la kuingizia majeneza. Jeneza lile lilipofika chini nikaona mwanamke aliye hai amezikwa na mumewe. Mwanamke yule nikamsaidia kutoka pale nikiwa na imani kuwa ana mikate yake saba ambapo huenda akanisaidia pindi ya kwangu ikiisha. Nikamsaidia kutoka pale na kujanae pembeni kabisa ya lile pango ambapo harufu za wafu hazifiki kwa kasi.
Siku ile usiku nilipolala ghafla nikasikia sauti ya mnyama anayechimba, nikasogea vizuri ila kwa kuwa ni kiza nisione vyema. Nikamwacha akaenda kule kwenye wafu na kuanza kula mizogo. Aple nilipo nikajisemea kuwa sasa huenda hii ndio nusura. Mnyama yule akala mizoga na muda wake ulipofika akatoka. Mimi nikawa namfatilia kwa nyuma usiku ule, tukapita njia nyembamba sana hatimaye akatokea baharini. Basi nikarudi tena kule pangoni kwenda kumchukuwa yule mwenzangu na kuchukuwa mali ambazo watu wamekuwa wakizikwa nazo kama mikufu ya dhahabu na thamani nyinginezo.
Nilibeba mzigo mkubwa sana wa mali za dhahabu na thamani nyingine nzuri. Tukatka mimi na mwenzangu yule na kwa bahati tukakutana na jahazi linaloelekea baghadad. Tulipanda mimi na mwenzangu yule. Tulipofika baghadad niliwahadithia kila kilichotokea na walishangaa sana kuniona nipo hai. Yule mwanamke nilompata kule nilisubiri eda yake ilipoisha kulingana na tamaduni za waislamu nikamwoamimi. Kwa hakika safari hii nimepata faida sana na mafunzo mengi.
Sin bad alipomaliza hadithi hii ya safari yake ya nne akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa awahikesho ajesikia yalompata kwenye safari ya tano. Safari hii ya tano kuna matukio kadhaa yalinikuta hivyo uwahi mapema. Kisha akampatia pesa kwa ajili ya matumizi ya siku ile na ijayo. Watu wote wakatawanyika.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 ai web app 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO.
Soma Zaidi...UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA
Soma Zaidi...SAMAKI WA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini.
Soma Zaidi...KUELEKEA BONDE LA UOKOZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUELEKEA BONDE LA UOKOZI Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi.
Soma Zaidi...HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA SAFARI SABA ZA BAHARIA SINBAD
SAFARI SABA ZA SINBADKatika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo.
Soma Zaidi...