Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HATITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDAD

 

Hapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana. Alikuwa ni kijana asiyepunguwa miaka 40, na alisifika kwa nguvu na akili sana na uwezo wa kufikiri alio nao. Alipendwa sana na watu na aliheshimika pia. Siku moja laikuwa amekaa eneo lake la kila siku kusubiri wateja, ghafla akatokea binti mmoja mrefu wa kiarabu. Binti huyu alimfanya mbeba mizigo amtazame sana kwa muda mrefu kwa uzuri alonao binti huyu. Binti akamwambia yule kijana nifate. Kwa haraka zaidi kijana akanyanyuka na kuanza kufata.

 

Wakafika kwenye nyumba moja yule binti akagonga mlango kwa madaha, mzee mmoja akatoka, binti akatia mkono kwenye mkoba wake na kutoa pesa nyingi na akampa yule mzee. Bila ya kuzungumza mzee alijiwa kinachotakiwa aliingia ndani na akaja na chupa kubwa lililojaa pombe. Kijana akabeba mzigo ule na kuuweka kwenye kapu lake kubwa la kubebea mizigo. Wakaelekea kwenye duka la matunda, hapa wakanunua matunda ya aina nyingi sana. Kisha wakafika duka lingine wakanunua vitu vingi sana vya harufu nzuri. Kwa urembo alonao huyu binti unaweza kufikiri ni vitu gani vya harufu nzuri angechukuwa. Kijana akamwambia “binti bora ungenambia toka mapema kama una mizigo mingi ili nichukuwe punda ama ngamia”. Binti akaheka sana na akamwambia “sijamaliza bado”.

 

Mambo yakawa hivyo waliendelea kununua vitu vingi katika matunda na vyakula na vinywaji. Vitu vya kunukia maua, mafuta pafyumu nna vinginevyo viingi. Wakafika kwenye nyumba mija mzuri sana, yule binti akaenda kuginja kwa madaha na upole zaidi kwenye malngo wa geti la nyumba hivyo. Muda wote kijana alikuwa akifurahia uwepo wa binti huyu na kila analofanya. Basi akatoka binti mwingine wa makamo aliyeonekana mzuri zaidi kuliko huyu na akafungua mlango.

 

Muda wote kijana alikuwa akishangaa na macho yake yaliganda kwa hutu mfungua mlango. Baada ya muda yule binti akamwambia “tafadhali ingia ndani”. Hapa kijana fahamu zikamrejea kwa shauku akaingia ndani. Alishangaa sana uzuri ulioje wa ndani pale. Nyumba yenye kila kizuri anachokijuwa na ambavyo ndo alianza kuviona. Kuna vinyago vya dhahabu na chemchem za maji. Meza yz almasi na sakafu yenye marumaru za kuvutia zaidi.

 

Kila kilichopo ndani hapa kilimflaisha kijana, ila zaidi ya hapo kilichomshangaza zaidi pale ndani kuna kiti kikubwa na zizuri. Aliyekaa kwenye kiti kile alikuwa ni dada mmoja mzuri sana huenda aliwashinda wote pale ndani. Kijana alifikiri yule ndo mkubwa wao, na huu ndo ukweli. Yule aliitwa Zubeida na yule alokuja nae kutoka kwenye bidhaa ni Sadie na yule alofungua mlango aliitwa Amina. Basi amina aliingiza mizigo ndani na sadie alitowa kiasi chapesa na kumpatia kijana.

 

Kijana aliendelea kushangaa pale ndani kwa muda mpaka zubeida akauliza “vipi kaka mbona hauondoki? Au unataka pesa zaidi?”. Kijana akaanza kujitetea kuwa angependa kukaa kidogo na akaleta hadithi nyingi na baadae wakamruhusu aendelee kukaa kidogo. Zubeida akamwabia “basi nitakuruhusu kukaa kwa sharti uwe mpole na usitowe siri ya maisha yetu hapa”. Kiana akakubaliana na sharti na akawajibu “nitatunza siri za humu ndani kuliko alivyotunza siri kinyozi wa mfalme”. Kwa shauku Amina akauliza “alifanya nini kinyozi wa mfalme?”. Kijana akamjibu amina “ni hadithi ndefu kidogo”. Akadakia Sadie “tusimulie basi hiyo hadithi ya kinyozi”. Kijana akamuangalia Zubeida aliyekuwa akimuashiria awaridhishe ndugu yake. Basi kijana akaanza kusimulia hadithi kama ifuatavyo

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1819

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

SAFARI YA KWANZA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA KWANZA YA SINBAD Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid.

Soma Zaidi...
Safari ya majibu juu ya maswali mawili

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.

Soma Zaidi...
SAMAKI WA AJABU

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini.

Soma Zaidi...
Kuelekea bonde la uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya binti mwenye kufichwa mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Alif lela u lela: utangulizi

Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru.

Soma Zaidi...