KUZALIWA KWA MTUME (S.A.W) NA MAISHA YAKE KABLA YA UTUME.
Mtume (s.a.w) alizaliwa siku ya juma tatu katika mweze rabil-awali (mfunguo sita) mwezi tisa (9) kwa mujibu wa wanahistoria katika mwaka wa tembo 571 B.K. baada ya kuzaliwa mama yake alituma mtu aende akatoe habari kwa mzee Abdul al-Muttalib juu ya kuzaliwa kwa mtoto. Kwa furaha kabisa alikuja mzee na akamchukuwa mtoto akambeba na kuelekea nae mbele za al-ka’aba (nymba tukufu ya Allah) kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu. Kisha akampa jina la Muhammad, jina ambalo halikuwa likijulikana na waarabu.

Kama ilivyo kawaida ya waarabu na jamii zingine wakati ule, Muhammad alinyonya kwa mama yake na kwa baadhi ya wanawake. Mtu wa kwanza kumnyonyesha Mtume baada ya mama yake ni Thuwaibah huyu alikuwa na mtumwa wa baba yake mdogo Abuu Lahab. Alivyonya Mtume Kwa Thuwaibah pamoja na mtoto wake Thuwaybah aitwaye Mosrouh. Pia Thuwaybah aliwahi kumvyonyesha Hamzah bin ‘Abdul-Muttalib na baadaye alimnyonyesha Abu Salamah bin ‘Abd Al-Asad Al-Makhzumi.