Kichaa cha mbwa.

Post hii inahusu zaidi kichaa cha mbwa,au kwa kitaalamu huitwa rabies, utokea pale mtu anapongatwa na mnyama ambaye ni jamii ya mtu au mbwa mwenyewe

Kichaa cha mbwa.

1.kichaa cha mbwa utokea pale mbwa anapomngata mtu  inawezekana akangata sehemu yoyote ya mwili inawezekana ukawa mkono , mguu yaani sehemu hiyo mbwa wanaachia virusi na ukaa kwenye kidonda kwa mda.

 

2. Baadae virus hao wanapitia kwenye mfumo wa Neva system, hasa hasa Neva zinazoelekea kwenye ubongo na virus wakishafika kwenye ubongo uhakikisha wameshambulia ubongo na hapo mtu ufanana kama amechanganyikiwa hivi na kuweza kuongea mambo yasiyofaa kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye ubongo.na hapo mgonjwa uweza kubwaka kama mbwa na pengine kuanza kuogopa vitu mbalimbali kwa mfano kuogopa maji.

 

3. Pia virus vikisha shambulia kwenye ubongo uendelea kuzaliana na kuongezeka na kuendelea kushambulia sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha mgonjwa kuwa na tabia kama za mbwa kabisa, pamoja na kubweka na mlio uweza kubadilika kuwa kama wa mbwa hapo mgonjwa hawezi kumaliza mda mrefu na kwa kawaida ufariki.

 

4. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kufahamu namna ya kichaa cha mbwa kinavyotokea na kuweza kutibu mapema au ikitokea mtu akangatwa na mbwa hata kama haujui kama mbwa ana kichaa au Hana ni lazima kuanza chanjo mara Moja kwa sababu chanjo zipo na zinapatikana kwenye hospital nyingi sana, kwa sababu ugonjwa huu unaua.

 

5. Na pia ni vizuri kabisa kuweza kuchanja mbwa mara kwa mara Ili kuweza kuepukana na tatizo hili linalopelekea kuhatarisha maisha ya watu, na pia chanjo ya kichaa cha mbwa ni ya gharama kweli ambapo kila chanjo ni sh elfu ishilini na tano na udungwa kwa mfululizo.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/25/Wednesday - 05:16:21 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1294


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-