Kazi za vitamin B na makundi yake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take
KAZI ZA VITAMINI B NA MAKUNDI YAKE
Vitamini B ni moja kati ya vitamini ambavyo vinahitajika sana mwilini. Athari yeyote ya upungufu wa vitamini hivi inaweza kuonekana moja kwa moja kwenye miili yetu. vitamini B vimegawanyika katika makundi mengi sana ikiwemo B1, B2, B3, B5, B6, B7, B9 na B12. je ungependa kujuwa kazi za vitamini hivi kulingana na aina zake. Endelea na makala hii upate kujifunza kazi za vitamini B.
Kazi za vitamini B kulingana na kila kundi la vitamini B
Basi tambuwa kuwa kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-
1. B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.
2. B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.
3. B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo
4. B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.
5. B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.
6. B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.
Kazi za vitamini B kwa ujumla
Kwa ujumla vitamini B vina kazi nyingi kama ulivyojifunza hapo juu. Kazi hizi tunaweza pia kuziweka katika ufupisho ufuatao. Lengo la kufupisha ni kukuwezesha msomaji kukumbuka kwa wepesi kazi za vitamini B. Kazi hizo ni kama zifuatazo:-
1. Husaidia mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema
2. Huhitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati (nguvu) mwilini
3. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mwilini
4. Husauidia katika utengenezwaji wa hemoglobin hizi ni chembechembe katika seli nyekundu za damu
5. Husaidia katika kuchakata DNA
6. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya na kukomaa kwa seli
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Madrasa kiganjani π4 Kitabu cha Afya π5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walio na majeraha ya macho.
Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Soma Zaidi...Aina mbalimbali za maumivu ya mwili.
Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali ya maumivu ya mwili, Maumivu ya mwili utokea kwa aina mbalimbali kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENGβATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.
Soma Zaidi...Upungufu wa damu mwilini
Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA.
Soma Zaidi...